Mkali wa Bongo Fleva ,Mr Blue amefunguka kuwa mke wake aitwaye Wahyda amemfanya aache kuvuta vilevi vyote vikali ikiwemo bangi,pombe,sigara,mirungi,n.k.

 Mr Blue amendika leo kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa.. Alhamdulilahi ..nimeamka salama nikiwa mwenye furaha ahsante mungu ..na nashukuru pia kwa kufaulu mtihani ahsante mke wangu @wahyda_bysers_heart kwa kunifanikisha kuacha vilevi vyote..(bangi, fegi, mirungi, pombe) na kuishi km binadamu wa kawaida..nawashauri ndugu zangu kuwa makini na marafiki wengine wapo kwa ajili ya kukuharibia maisha yako ..kuwa makini
 
Top