Umezisoma Hizi?
Loading...
http://bit.ly/1obie07

HABARI MPYA

no image

UKWELI WOTE KUHUSU ISHU YA CHID BENZ KUTEMBEZA KIPIGO KWA MREMBO. SOMA HAPA.


MAJANGA! Msanii wa Hip Hop anayetokea Ilala, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ amedaiwa kumpa kipigo kizito mpenzi wake wa zamani aliyefahamika kwa jina la Mwanaisha Kiboye.
Rashid Makwiro ‘Chid Benz’.
Tukio hilo lililokusanya umati wa watu lilijiri Jumapili iliyopita maeneo ya Buguruni (kwenye mafleti) jijini Dar ambapo Chid alikuwa kwenye mizunguko yake na mpenzi wake wa sasa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

ISHU ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Chid na mpenzi wake huyo walifika katika baa moja maarufu iliyopo katika mafleti hayo na kumkuta Mwanaisha akiwa amekaa na rafiki zake. Demu huyo alimsalimia Chid na ndipo mtiti ukaibuka.

“Mwanaisha alipomuona Chid anakatiza na kwa kuwa aliwahi kuwa mpenzi wake, akaona siyo ishu bora ampe hai kwa mbali ndipo Chid alipomaindi na kumfuata huku akisema: unajifanya unanijua sana siyo? Ngoja nikuoneshe,” kilisema chanzo.  

AMZIMISHA
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Chid kusema hivyo alimshushia kipondo kikali hasa sehemu za usoni na kumsababisha Mwanaisha achanike mdomoni kabla ya kuzimia palepale na kuanza kupepewa na marafiki zake, Chid akatokomea kusikojulikana.

Imeelezwa kuwa, Mwanaisha alipozinduka baada ya kupepewa alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Pangani, Ilala ambapo alipewa Fomu ya Polisi Nambari 3   (PF3) kisha kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu, Ilala - Amana. 

CHID NAYE AKIMBILIA POLISI
Chanzo kimezidi kueleza kuwa, wakati Mwanaisha akianza kupewa matibabu hospitalini, Chid naye alishauriwa na marafiki zake kwenda kutoa taarifa katika kituo hicho cha polisi kama njia ya kujihami pasipo kujua kuwa  ameshawahiwa.
 

“Marafiki zake walioshuhudia tukio hilo walimshauri jamaa (Chid) akafungue mashitaka polisi kama njia ya kujihami, akakubali ndipo alipokwenda kutiwa nguvuni kwani tayari Mwanaisha alikuwa ameshamuwahi,” kilisema chanzo hicho.  

ATUPWA MAHABUSU
Habari zimeeleza kuwa, Chid alipofika kituoni kwa ajili ya kutoa taarifa, alidakwa na kusokomezwa mahabusu kwa vile tayari alikuwa ameshafunguliwa mashitaka.
 

Chanzo kilichopo polisi hapo kimeliambia Amani kuwa, jamaa alipoambiwa avue mkanda ili atupwe sero alileta ubishi hivyo kusababisha polisi watumie nguvu ya ziada kumdhibiti kwa sababu alisema yeye ni mtu maarufu hivyo hawawezi kumtisha.  

AKUTWA NA BANGI
Wakati msanii huyo anayesifika kwa  sauti nzito akitaka kuingizwa ndani, alisachiwa na kukutwa na misokoto miwili ya bangi hivyo kuandikishwa kesi nyingine ya madawa ya kulevya mbali na ile ya awali ya kujeruhi.
 

MWANAISHA ANASEMAJE?
Juzi Jumanne, Amani lililimsaka Mwanaisha ambapo lilifanikiwa kumkuta nyumbani kwao, maeneo ya Sharifu Shamba,  Ilala akiwa hawezi kutembea, kuongea vizuri akiwa hoi kitandani.
Akizungumza kwa shidashida, Mwanaisha alisema anasikitika kuona Chid amempiga bila kisa.

“Sijui hata kwa nini aliamua kunipiga, amenipiga vibaya, nimeshonwa nyuzi 12 na bado nasikia maumivu makali kichwani,” alisema. 

Kwa mujibu wa dada wa Mwanaisha ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, watafuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo ili kuona mwisho wake kwani mbali na kumweka majeraha ndugu yake lakini bado hali ni mbaya na wanatakiwa kumfanyia Kipimo cha CT Scan. 

“Hizi gharama zote tutakazohangaika kumtibu ndugu yetu lazima Chid azilipe maana amempiga ndugu yetu pasipo kufanya kosa lolote,” alisema dada wa Mwanaisha.  

APANDISHWA KIZIMBANI
Kwa kuwa Jumapili na Jumatatu ilikuwa Sikukuu ya Pasaka, juzi Jumanne Chid alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo - Ilala na kusomewa mashitaka mawili; KUJERUHI na KUKUTWA NA BANGI.
 

Siku hiyo, mahakama ilimsomea mashitaka na kutakiwa kujibu kama ni kweli amefanya makosa hayo lakini mshitakiwa huyo alikanusha makosa yote mawili hivyo kesi hizo kuahirishwa.
KESI ZATOFAUTISHWA
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mahakama hiyo, kesi ya kujeruhi inatarajiwa kutajwa tena mahakamani hapo Aprili 24, mwaka huu (leo) huku ile ya kukutwa na bangi ikisogezwa mbele hadi Mei 6, mwaka huu.
 

APATA DHAMANA
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hizo, mshitakiwa alipewa nafasi ya kupata dhamana kwa masharti ya kulipia shilingi 100,000 huku akidhaminiwa na watu wawili ambapo Chid alitimiza masharti hayo na kuachiwa huru kusubiri kesi zitajwe tena.

Kamanda wa Mkoa wa Polisi Ilala, ACP Marieta Minangi amekiri kutokea kwa tukio hilo.
BOFYA PLAY HAPA CHINI KUCHEKI VIDEO HIYO
UTAJIRI WA IRENE UWOYA WAZUA UTATA, HAIJULIKANI PESA ZAKE ZINAPOTOKEA. SOMA HAPA

UTAJIRI WA IRENE UWOYA WAZUA UTATA, HAIJULIKANI PESA ZAKE ZINAPOTOKEA. SOMA HAPA

Inadaiwa kuwa hali ya hewa imechafuka kwa msanii nyota wa filamu za Bongo Irene Uwoya ambapo ameshindwa kutaja vyanzo vya utajiri wake wa Ghafla, Hivi karibuni Uwoya alikaririwa akisema kuwa hawezi kutaja kazi nyingine anayofanya na utajiri aliokuwa nao kwani wapo baadhi ya watu hawapendi kuona mmoja wao akiendelea ...Alisema kuwa pamoja na magari anayomiliki ya kifahari hawezi sema ni njia gani amepata utajiri huo..Nimefanya Filamu kadhaa ambazo zimenipa hela na cha zaidi ni Jina ambalo limenifanya kupata Deals zingine zinazonipa Pesa..Jina langu ni Kubwa so lazima liendane na Mali ninazopata.....
LAZIMA UKUBALI TU..!! HUU NDIYO UJIO MPYA WA OMMY DIMPOZ BAADA YA TUPOGO, TAZAMA VIDEO HAPA..!!

LAZIMA UKUBALI TU..!! HUU NDIYO UJIO MPYA WA OMMY DIMPOZ BAADA YA TUPOGO, TAZAMA VIDEO HAPA..!!

Ommy Dimpoz a.k.a Poz kwa poz ameamua kuwaonjesha kionjo cha wimbo wake mpya unaokuja ambao video yake imefanywa nchini Marekani Na producer mkali nchini humo.
Kupiti Account yake ya Instagram Ommy dimpoz aliweka kionjo cha Video hii na kusema ndio cha wimbo huo unaosubiriwa na Wapenzi wa Muziki wa Bongo fleva Kwa Hamu Kubwa.
CREDIT : LINDI YETU

Sikiliza Na kumtazama Hapa:
no image

BREAKING NEWS : BOMU LALIPUKA KENYA NA KUUWA POLISI NA ABIRIA WALIOKUWA NA BOMU HILO


BREAKINGNEWS
Bomu linaripotiwa kulipuka kwenye gari na kuuwa watu wanne ikiwa ni Polisi wawili na abiria wawili ambao wanashukiwa walikuwa na bomu hilo kwenye gari karibu na kituo cha Polisi cha Pangani.
Lakini ilivyotokea inaripotiwa na gazeti la Starndard kwamba Polisi hao wawili waliwakamata washukiwa waliokuwa na kuamua kuwapeleka kituo cha Polisi wakiwa na bomu hilo kwenye gari!
Kabla ya kufika kituoni bomu hilo lilipuka na kuuwa wote Polisi pamoja na washukiwa ambao walikuwa kwenye jaribio la kujitoa muhanga.Haijajulikana mara moja kwanini Polisi hao waliamua kuchukua hatua ya namna hii lakini habari zaidi baadaye..
no image

HII NDIO BARUA NZITO KUTOKA GPL KWENDA KWA LULU, UNAWEZA ISOMA HAPA

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
KWAKO Elizabeth Michael ‘Lulu’. Leo nimeona nikukumbuke kupitia barua! Natambua uwezo wako mkubwa katika kazi, juhudi zako binafsi ndiyo zimekufikisha hapo ulipo, mataifa mbalimbali sasa wanatambua kuwa kuna mtu anaitwa Lulu, yupo Bongo, muigizaji!.
Sitaki kukurudisha sana nyuma lakini najua unajua kuwa ni jinsi gani kipindi cha nyuma ulikuwa ukipamba vyombo vya habari kwa skendo chafu. Ulipoteza dira ya kimaisha, watu wengi waliokuwa wakikufuatilia kazi zako walianza kukutupa.
Walikupotezea kwa sababu ya matukio ya ulevi, mavazi ya nusu utupu na matukio mengi ya ajabuajabu yaliyofanana na hayo. Sina nia mbaya kukumbusha lakini waswahili wanasema binadamu anajifunza kutokana na makosa. Maishani mwako umekutana na mazito yasiyofanana na umri wako.
Kwenye ulimwengu wa mahaba, ilikuwepo minong’ono mingi juu ya watu wanaotajwa kushiriki mapenzi na wewe, walitajwa vigogo, mastaa na hata wasio mastaa. Sitaki kusema ni kweli au la lakini lisemwalo kama halipo, ujue laja.
Siri ilifichuka kupitia kifo cha yule unayedai alikuwa mwandani wako, marehemu Steven Kanumba.
Mazingira ya kifo chake, umri mdogo uliokuwa nao ilikuwa ni fundisho kubwa maishani mwako. Ulipambana na msalaba wa gereza, ukapambana na mlolongo wa kesi mahakamani hadi pale ulipofanikiwa kutoka kwa dhamana, Januari mwaka jana.

Baada ya kutoka mahabusu, kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja sasa ulikuwa kimya, ulionekana kubadilika kitabia. Yale uliyokuwa ukiyafanya awali, uliyaweka pembeni na zaidi kusimamia mustakabali mzima wa maisha yako, ulikuwa mwema sana aisee!.
Kinachonisikitisha ni kuanza kusikia tena matukio ya ajabu, unaonekana kubadilika. Nimefuatilia tabia zako, naona umeanza kubadilika, umesahau eeeh! Mavazi yako kwa miezi michache iliyopita, nimegundua yanaanza kuchepuka! Mfano mzuri ni kigauni ulichokivaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe yako ya kuzaliwa.
Hakikustiri maungo yako nyeti, kilionesha sehemu kubwa ya matiti yako.
Kama hiyo haitoshi, kupitia mitandao ya kijamii umeanza kushusha matusi mazito bila sababu za msingi, mtu akikukosoa kidogo, unampa maneno machafu ambayo hayaandikiki gazetini. Kama kioo cha jamii, unapaswa kuvumilia mengi.

Nikiwa kwenye kazi zangu za kila siku, huwa nakuwa wa kwanza kupata fununu za mabadiliko ya kila msanii na namna anavyoishi. Nikuonye tu, kuwa makini na mwenendo wako kwani tayari jamii ilishaanza kujenga imani na wewe. Uliaminika na ndiyo maana ukapata bahati ya kuchukuliwa katika kampuni nzuri ikakusimamia kazi zako hadi sasa.
Kwa kuwa tayari nimeanza kupata malalamiko kutoka katika vyanzo vyangu, nikusihi sana mdogo wangu, usirudi ulipotoka. Jenga heshima mpya na jamii ikuamini kutokana na kazi zako na si skendo za ajabuajabu, kwa leo ni hayo tu!
Wasalam.
Ni mimi Anko Erick Evarist.

GPL
no image

JACK PATRICK AANGUA KILIO KORTINI HUKO CHINA, N BAADA YA KUTOKUEPO KWA MBONGO MMOJA MAHAKAMANI. HATA JUX KASEPA

HATIMAYE modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ amepandishwa kortini kwa mara ya kwanza huko Macau nchini China, Aprili 10, mwaka huu kwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 huku ishu kubwa kwa muda wote aliokuwa mahakamani ikiwa ni kuangua kilio kila wakati.
Kete zinazosadikiwa kukutwa na modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ akiwa amezimeza.
Jack alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Desemba mwaka jana akitokea Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo.
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua hiyo dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za Wachina tu zikimwangilia.
Jack akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kunaswa.
“Yeye alijua angekuta Wabongo au hata watu weusi wakimpa kampani, lakini matokeo yake alikutana na sura za Wachina tu,” kilisema  chanzo chetu.
Kikaendelea: “Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo.”
DAKIKA 10 ZATUMIKA KUMSOMEA MASHITAKA
Kuna madai kwamba, msoma mashitaka wa mahakama hiyo alitumia dakika 10 kutokana na taratibu za kisheria za huko huku akitakiwa kusema ndiyo au hapana tu kabla keshi hiyo kupigwa kalenda hadi Mei 23, mwaka huu.

Jack akiwa karibu na madawa aliyonaswa nayo.
KUNA MADAI ALIZOMEWA
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke huo mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa nchi hiyo walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini.
Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au kumsema vibaya mtu aliyedakwa na madawa ya kulevya ni kawaida kwani hakuna biashara, inapigwa vita nchini humo kama ya unga wakiamini unaangamiza nguvu kazi ya kizazi kijacho.
NDUGU WADAIWA KUMKATIA MAWASILIANO
Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.
“Unajua ndugu zake walikata mawasiliano kabisa? Nchi nzima au tuseme dunia nzima kilio ni jinsi vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule kubainika kwamba Jack alibeba unga tumboni kwenda kuuza kumeifanya familia kujisikia vibaya sana,” kiliongeza chanzo hicho kikiomba chondechonde kisitajwe gazetini.
Jack Patrick.
KAMA ATARUDI BONGO SALAMA
Habari zaidi zinadai kwamba modo huyo ambaye pia ni Miss Ilala No 3, 2005, aliwahi kumwambia mshirika wake mmoja akiwa mahabusu kwamba, kama atabahatika kurejea Bongo salama,
atakwenda kupiga dua juu ya kaburi la mama yake ili amsimamie katika kumwondolea nuksi kama siyo mabalaa. Baba wa Jack anadaiwa kuishi nje ya nchi.
TUJIKUMBUSHE
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China ambako ilidaiwa ndiko alikokuwa anafikisha unga huo.
Ilidaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kukamatwa kwake ni kuonesha uso wenye uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria, yaani ‘passport’ kukutwa imegongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara jambo ambalo wakaguzi waliliona si la kawaida kwa msichana kama yeye.
GPL
no image

AL SHABAB WATISHIA KUWALIPIA KENYE TENA, HIKI NDO WALICHOKISEMA. SOMA HAPA

TZA KENYA YATISHIWA NA ALSHABAABTishio la kigaidi lina kodolea macho taifa la Kenya baada ya kundi la kigaidi lililo na makao yake makuu nchini Somalia kuachia video nyingine kwenye mtandao wa Al-Kataib wakitishia kutekeleza mashambulizi nchini Kenya wakati wowote.
kwenye kanda hiyo msemaji wa alshabaab aliye jifunika uso anasema kwamba hawaoni lolote litakalo wa zuia kuingia Kenya hasa baada ya kufanikiwa kutekeleza mauaji katika jengo la west Gate. mwaka uliopita>>’tumekuwa tukisema tutafika Kenya lakini hivi tayari tushafika si eti westgate ndio tosha bado kuna mamia na mamia ya watu wanaongojewa mahala kama hiyo insha Allah’alisema msemaji huyo.
Huku wakiimbia tutawalipua hadi tuwamalize wanamgambo hao wamesema kwamba wameamua kuungana na wasomali kutetea dini ya Allah,Wadadisi wa maswala ya kiusalama wanahoji kwamba huenda hawa ni baadhi ya vijana kutoka kwa mataifa ya Afrika mashariki walipewa mafunzo ya itikadi kali na baadaye kupelekwa somalia kujiunga na Alshabaab kutokana na wanavyozungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kwenye video hiyo.
Ispekta mkuu wa polisi nchini Kenya bwana David kimaiyo amesema uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha video hiyo na taarifa kamili kutolewa punde tu watakapo pata habari zaidi kuhusiana na video hiyo.
.
Bofya hapa kututumia ujumbe
Press Esc to close
Copyright © 2013 BongoClan™ All Right Reserved