Shindano la Fanya Kweli Kiwanjani
limefikia tamati kwa jiji la Dar es salaam huku wapenzi wa bia ya Tusker wakishuhudia
baa ya Kinondoni M.K Pub ikiibuka kidedea baada ya kuzibwaga baa nyingine 9
zilizokuwa zinachuana kwenye shindano hilo.
Shamrashamra za kuipongeza baa hiyo zilipambwa
na burudani ya muziki kutoka kwa ma Dj wa redio E-fm na watangazaji wa kituo
hicho waliojumuika na mameneja wa bia ya Tusker kuipongeza baa hiyo.
Uchangamfu wa kiwanja hicho uliongezeka
zaidi mishale ya saa moja jioni baada ya wadhamini wa shindano hilo kuanza
kutoa zawadi kwa wateja wa bia ya Tusker waliofuruka kiwanjani hapo.
Kwa upande wake Bw. Francis Kimbona mteja
wa siku zote kiwanjani hapo alitoa pongezi kwa wadhamini wa shindano hilo kwa
kuanzisha kitu chenye lengo la kukuza zaidi mauzo ya baa mbalimbali za mitaa
tunayoishi.
“Mashindano kama haya ni muhimu kwa kukuza
kipato cha hizi baa zetu na niwaombe tu wadhamini waendelee kuonyesha mfano kwa
jamii” aliongeza Bw. Kimbona.
Naye meneja wa bia ya Tusker Bi. Sialouise
Shayo hakusita kuipongeza baa hiyo kwa kuibuka na ushindi huku akiwashukuru
wateja wa bia hiyo kwa kuonesha uzalendo pale walipoombwa kuzipigia kura baa
zote 50 zilizoorodheshwa kwenye shindano hilo.
“Tumepokea ushiriki mkubwa kutoka kwa
wadau wakati wote wa shindano hili zaidi ya vile tulivyotarajia, hivyo nitoe tu
pongezi kwa wateja wote wa bia ya Tusker walioshiriki katika kuzipigia kura baa
za mitaa wanayoishi ili kuziwezesha zishinde shindano hili.” aliongeza Bi
Shayo.
Kampeni hiyo ambayo imedumu kwa takriban
muda wa wiki tano imekua na lengo la kuziibua baa mbalimbali za mitaa
tunayoishi na kuzitangaza kwa wadau wa kinywaji cha Tusker ambapo wadau hao
walipewa jukumu la kushiriki kuzipigia kura baa zetu pendwa ili zishinde
shindano hilo.
Kupitia bia ya Tusker mameneja wa kinywaji
hicho waliweza kuorodhesha baa 50 kwenye shindano hilo ambapo kwa muda wa wiki
tano wa kampeni baa 10 zilipata kuchuana vikali kila wiki ili kuweza kumpata
mshindi mmoja tu. Hivyo basi ndani ya wiki tano za shindano baa ambazo
ziliibuka kidedea ni pamoja na;- “Toroka uje ya Kimara-Korogwe, Yenu bar ya
Ubungo-Maji, New Jambo bar ya Mabibo, Kilwa road Pub ya Kurasini na “MK Pub ya
Kinondoni iliyofunga shindano hilo.
Shindano hilo limefikia tamati kwa mkoa wa
Dar es salaam huku mipango ya kulisogeza mikoani pia ikiendelea kuwekwa vizuri.
Kwa taarifa Zaidi tembelea;
Kurasa za facebook Tusker Tanzania na
Twitter @Tusker Tanzania