Msanii wa Bongo Movies, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ aliyewahi kuripotiwa kujiachia kimahaba na mwanamuziki Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ ametia aibu kubwa baada ya picha zake za utupu kuzagaa mitandaoni.
Kutokana na picha hizo ambazo zimeonekana kuzagaa katika mitandao
mbalimbali na kuacha viulizo kwa wasanii wengi wanaomfahamu, mwandishi
wetu alimtafuta Bozi ambaye alionekana kutafunatafuna maneno na kumtupia
lawama nzito Nay wa Mitego ambaye aliwahi kumtumia picha hizo
walipokuwa wapenzi.