Meneja huyo, Aidan Seif alisema video hiyo ipo katika matengenezo nje ya nchi.
“Awali tulikuwa tumepanga ifanyike Afrika Kusini,
lakini kutokana na machafuko tuliahirisha, ikatakiwa ifanyike nchi
nyingine Afrika. Kilichochelewesha kwa sasa ni upatikanaji wa vibali
kuingia Marekani kwa ajili ya shoo na mambo mengine, lakini
tumeshafanikiwa kukamilisha taratibu hizo na wiki hii itafanyika,”
alisema Aidan akiashiria kuwa picha za video hiyo zitachukuliwa
Marekani.
Alifafanua kwamba taratibu mbalimbali zinaendelea,
hivyo kesho (Alhamisi iliyopita) atazungumza jambo kuhusu hatima ya video hiyo na
ni lini hasa itatolewa.
Mwanzoni mwa wiki, mashabiki mbalimbali wa Ali
Kiba walianza kuhoji kupitia picha aliyoiweka nyota huyo wa muziki wa
kizazi kipya katika mtandao wa kijamii wa instagram wakilalamikia
ucheleweshwaji wa video hiyo na kudai kwamba anawaangusha.
“Kuna kitu watu wanashindwa kukikubali hapa. Ali
Kiba anakabiliwa na pressure hii sababu ya kushindanishwa na Diamond.
Mimi si muumini wa hizi team, lakini kama mchambuzi wa muziki na mtu
ninayefuatilia sana muziki wa Tanzania, napenda watu watambue na
kukubali kuwa Diamond na Ali Kiba hawako sawa tena. Mnamuonea tu Kiba
kumfananisha na Diamond,” aliandika shabiki mmoja anayetumia jina la
Kyusho katika mtandao huo.
“Hebu fikirieni mwenzie baada ya kutoa video ya
wimbo wa “Nasema Nao”, ametoa video nyingine mbili tena akiwa na wasanii
wakubwa Afrika na “Nakupenda” aliyorekodi na Iyanya, lakini Kiba bado
anadaiwa video moja tu ya “Cheketua”. Ni kweli anawaangusha sana
mashabiki wake, lakini pengine huo ndiyo uwezo wake hivyo kwa kumtegemea
afanye kama Diamond mnamuonea tu!”
Gazeti la Mwananchi
Gazeti la Mwananchi