BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???


Miaka 1065 iliyopita katika siku kama ya leo, inayosadifiana na tarehe 20 Dhulqaada mwaka 370 Hijria, alizaliwa Abu Ali Sina mwanafalsafa na tabibu mashuhuri wa Kiislamu na Kiirani aliyejulikana pia kwa laqabu ya Sheikhul Rais. Ibn Sina alihifadhi Qur'ani yote alipokuwa na umri wa miaka 10. Ibn Sina alijifunza utabibu baada ya kupata elimu za mantiki, hisabati, nujumu, falsafa pamoja na elimu nyinginezo. Alianza kuandika vitabu akiwa na umri wa miaka 21 na miongoni mwa vitabu vyake maarufu ni Qanun, Shifaa na Isharaat.
Siku kama ya leo miaka 278 iliyopita Daniel Gabriel Fahrenheit mwanahesabati na mwanafizikia wa Kijerumani aliyevumbua kipimajoto alifariki dunia akiwa na miaka 50. Fahrenheit alikuwa na fikra ya kubuni kifaa kitakachokuwa na uwezo wa kupima kiwango cha joto na ndipo mwaka 1724, msomi mwanafizikia huyo wa Kijerumani alipofanikiwa kutengeneza kipimajoto (thermometer). Kifaa hicho bado kinatumiwa hadi sasa na aina ya nyuzi joto za chombo hicho imepewa jina la msomi huyo mwenyewe yaani Fahreinheit. Daniel Gabriel Fahreinheit aliaga dunia mwaka 1686.
Miaka 83 iliyopita mwafaka na siku hii ya leo, aliuawa Omar al Mukhtar kiongozi wa taifa la Libya katika mapambano dhidi ya wakoloni wa Italia. Omar Mukhtar aliyekuwa kiongozi wa kidini alizaliwa mwaka 1859. Mwaka 1895 alielekea Sudan na kushiriki katika harakati za kupambana na ukoloni wa Uingereza. Baada ya kushindwa kwa harakati hizo Omar Mukhtar akalazimika kurejea nchini Libya. Mwaka 1911 Wataliano wakiwa na lengo la kuitawala Libya walianzisha vita na dola la Uthmania. Kiongozi huyo wa kidini aliwahimiza wapiganaji wa makabila ya Libya kusimama kidete na kupambana dhidi ya wavamizi wa Kitaliano. Hata hivyo kwa kutumia askari wengi zaidi na silaha za kisasa wavamizi hao wa Kitaliano walimzingira Omar Mukhtar na wenzake na kumkamata na kisha wakamnyonga katika siku kama ya leo.
Na siku kama ya leo miaka 36 iliyopita, zilzala iliyokuwa na ukubwa wa 7.7 kwa kipimo cha rishta ililitikisa eneo la kaskazini mashariki mwa Iran na kuuharibu mji wa Tabas na vijiji vya kando kando yake. Watu zaidi ya elfu 25 waliuawa na makumi ya maelfu kujeruhiwa katika mtetemeko huo mkubwa wa ardhi. Zilzala ya Tabas ilitokea sambamba na kupamba moto mapambano ya wananchi wa Iran dhidi ya utawala wa Shah.