Sherehe za wafanyakazi (Mei mosi) zinasimamiwa na vyama vya wafanyakazi zikiratibiwa na TUCTA.
Sherehe za wafanyabiashara sabasaba zinaratibiwa na TANTRED NA TCCIA.
Sherehe za wakulima (wakulima, wafugaji na wavuvi) zinaratibiwa na TASO
Mh.Raisi/
waziri mkuu upo uvumi ulionea na uliotangazwa na katibu mkuu wizara ya
kilimo,ufugaji na ushirika kwamba chama cha TASO kimefutwa na
maadhimisho ya sherehe ya wakulima (NANENANE) ziratibiwe na watumishi
(sekretarieti za mikoa).Kwa nini Mh.Raisi/waziri mkuu kama chama cha
TASO kimefutwa kwa nini sherehe za nanenane zisifutwe?
kuliko kusimamiwa na wasiohusika.
Sisi
wanachama wa TASO tumesikitishwa sana na jambo hili kwani hatuelewi
chama chetu kimefutwa kwa taratibu zipi,mbona hatujashirikishwa kupitia
vikao vyetu kwa mujibu wa KATIBA ?
Pamoja nakuwepo
au kutokuwepo jambo hili hivi vyama vya wafanyakazi vikifutwa TASO Au
TANTRED wanaweza kuratibu nakusimamia sherehe za wafanyakazi?. Kinachotusikitisha zaidi hao watumishi wa UMMA walioteuliwa kuratibu nakusimamia wana WELEDI kiasi gani na shughuli za wakulima?
Mh
Raisi/waziri mkuu sisi wakulima ambao ndio kundi kubwa nchini
tunanyanyasika sana na hawa watumishi wa UMMA ambao hujiona kwamba wana
WELEDI mkubwa kuliko sisi wakulima kama ambavyo msajili wa vyama hiari
(mambo ya ndani)alivyoamua kwa makusudi kutofuata taratibu nakufuta
chama chetu bila kutushirikisha kwakua sisi ni mambumbumbu kama
wanavyotuita kitendo ambacho tunakilaumu sana .Mh .Rais/Waziri mkuu hawa
sekretarieti zamikoa wametupangia viingilio vikubwa kuingia kwenye
viwanja ambavyo ni mali yetu TASO mfano kiingilio uwanjani mtu mzima
Tshs 2000/ na mtoto 1000/ hivi Mh tunaenda kufanya biashara au
kujifunza mbona wenzetu wafanya kazi wanapopeleka matatizo yao kwako
huingia bure?
uwanjani?
Jambo
jingine ni kwamba sisi TASO tulikua tunatoa kiingilio kidogo kupata
pesa zakuendesha chama je hizi sekretarieti za mikoa hizo fedha
watakazokusanya wanapeleka wapi?
Jingine Mh .hawa
watumishi walioteuliwa kuratibu shughuli za NANENANE wametoka kwenye
vituo vya kazi takribani mwezi kuanzia tarehe 01/07/-9/8/2012 je
wananchi wanapata wapi huduma zao na kauli mbiu ya awamu ya TANO ni HAPA
KAZI TU,sasa kusimamia sherehe za nanenane ni kazi inayowalipa
mishahara na huku wanalipwa posho kila siku je nisahihi.
Tunafikisha
kilio chetu kwako juu ya swala hili kwani wewe ndio Mkombozi Wetu
wakulima tumechoka kunyanyasika hasa katika awamu ya Utawala wako.