Miss Tanzania wa mwaka 2000 na mwanamuziki wa bongo fleva, jackline
ntuyabaliwe aka k- lyn hatimaye amekuwa mke mke rasmi wa mfanyabiashara
maarufu na TAJIRI nambar moja nchini, Reginald mengi baada ya kufunga
ndoa iliyohudhiriwa na mastaa mbali mbali wa nchini ufaransa na
Tanzania.
Kama ilivyo ada kwa mke wa raisi kuitwa "FIRST LADY vivyo hivyo kwa mke
wa tajiri jina hubadilika na kuwa "BOSSLADY ". Kutokana na hali hiyo
kuanzia sasa k-lyn anakuwa ndiye raisi wa ma bosslady wote afrika
mashariki kutokana na pesa aliyonayo mumewe mzee reginald mengi.
Awali kabla ya k-lyn kutwaa wadhifa huo, mwanamuziki na mfanyabiashara
toka uganda ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki nguli wa bongo fleva diamond
platnumz, zarinah hussein aka zari aliaminika ndiye anayeongoza kwa
pesa kwa mastaa Africa mashariki. Kwa sasa hali imebadilika na taji hilo
kuelekea kwa mwana mama mrembo K -lyn.