Mkwere awatolea uvivu wasanii wenzake, asema haogopi kurogwa.
“Mimi nasema tu, siogopi kurogwa bwana utaniroga wewe mimi narogwa na watanzania wengi ninaowafurahisha kila siku, nasema wasanii tubadilike katika kujitenga katika matukio kama maradhi, misiba na sherehe tushirikiane tupendane,”anasema Mkwere.
Mkwere alisema hayo wakati akiongelea suala la baadhi ya wasanii kujitenga na wasanii wenzao kwa mitazamo ya kipato, au makundi makundi ambayo kwake haoni kama yana nafasi katika maisha ya wasanii wa filamu na komedi ambao siku ya siku wote ni kitu kimoja kwani hawana tofauti sana kiubinadamu.