Jana ndipo ilipokuwa safari ya mwisho ya Marehemu Mzee Sykes baba yake na Msanii Mkongwe Nchini Dully Sykes ambapo Mzee Sykes alipumzishwa katika makazi yake ya Milele huko katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar-es-Salaam.
Kutokana na Msiba huo Tokea Juzi simu ya Dully Imekuwa haipatikani Ila leo @DjHaazu wa @MamboJamboRadio amempata na Kupiga naye Story mbili tatu kuhusiana na Marehemu Mzee Sykes kwa kifupi.
Katika Mazungumzo yake Dully ameeleza kuwa Mzee Wake alikuwa anaugua Muda mrefu na kilichopelekea kifo chake ni uvimbe Miguuni ambao ulipelekea Kutengeneza sumu mwilini na Hatimaye kupelekea Sumu hiyo kuzima Taa Angavu.
Matumizi ya Sigara nayo Amesema ni Chanzo cha Kifo cha Mzee Sykes japo ameugua ile Serious kwa wiki Mbili.
Kwa upande M,wingine Dully amesema kuwa Tofauti na Damu ya Mzee Kumzaa lakini Baba yake ana mchango Mkubwa sana Katika Maisha yake ya Muziki na Ana nafasi kubwa sana ya Pale Dully alipo hadi leo hii.
UNAWEZA KUMSIKILIZA DULLY AKIONGEA NA HAMIS ABTWAY MAARUFU KAMA @DjHaazu KWA KUCLICK HAPA:> @DJHAAZU__DULLY - AELEZEA MCHANGO WA BABA YAKE KWENYE MUZIKI WAKE