
Waziri wa nishati na Madini, Profesa sospeter Muhongo, ametangaza kujiuzulu kutoka wadhifa huo mapema leo Jumamosi Januari 24, 2015. Waziri huyo mtaalamu wa miamba, amejiuzulu kufuatia shinikizo la muda mrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya bunge lililopita, lililoagiza serikali kuchukua hatua dhidi ya wateule wake, kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow. Waziri Muhongo ametangaza uamizi huo mbele ya waandishi wa habari kwenye makao makuu ya wizara ya Nishati na Madini, barabara ya samora katikati ya jiji la dar es Salaam..........mengi zaidi yatafuata - See more at: http://mwanaharakatimzalendo.blogspot.com/2015/01/breaking-news-prof-muhongo-kajiuzulu.html#sthash.RfkcvVE4.dpuf