Wema Sepetu akiwa na Kope Bandia
Stori: Imelda Mtema/Risasi
BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa anajuta kutumia kope za bandia kwa muda mrefu kwani zimeharibu kope zake za asili.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema alisema awali alikuwa hawezi kutoka kwenda kokote bila kuweka kope hizo na hata asipozibandika anajisikia vibaya lakini baada ya kumharibia muonekano wake wa asili, hataki hata kusikia.

“Jamani hakuna kitu ambacho nimekichukia kwa hivi sasa kama kope za bandia sina tena ushawishi nazo kabisa zimeharibu macho yangu, situmii tena,” alisema Wema.
GPL
 
Top