BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???

Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (Kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya microwave ambayo inatolewa kama zawadi kwa wateja wanaonunua friji za kisasa za LG. Tukio hilo lilifanyika katika banda la LG ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama Sabasaba, wa pili kushoto ni meneja wa tawi la LG Mtaa wa Nkurumah ,Yasin Lodhi .

Bw. Festo Sakaya akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea zawadi ya Microwave ya kisasa toka LG ambayo aliipata baada ya kufanya manunuzi ya friji la kisasa ndani ya banda la LG wakati wa maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama Sabasaba.

Meneja wa tawi la LG Mtaa wa Nkurumah, Yasin Lodhi, (kulia) akikabidhi zawadi ya Microwave kwa Bi. Hidaya Kapera, (kushoto) mara baada ya mteja huyo kufanya manunuzi ya bidhaa za kisasa ndani ya banda la LG katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba.

Hidaya Kapera, akiondoka na zawadi yake ya Microwave baada ya kufanya manunuzi ya bidhaa za kisasa ndani ya banda la LG katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba.

Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuendesha promosheni katika banda la LG na watu kujishindia zawadi mbalimbali kama:-Microwave na fulana katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya LG wakimpongeza Bw. Festo Sakaya kushoto baada ya kushinda zawadi ya Microwave katika promosheni iliyoendeshwa na kampuni hiyo katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba.