Baada ya Video mpya ya Ommy Dimpoz Kutoka Jana Baadhi ya
Watu wakiwemo bloggers Maarufu kama U-turn Wameendeleza kuponda tunzi na
melody za nyimbo zinazotolewa hivi sasa hasa kutoka kwa wanamuziki
wakubwa ..Tukija kwenye hii nyimbo mpya ya Ommy Dimpoz ya Wanjera Wengi
wamesema hakuna jipya kwenye wimbo na mashairi ila Video imetokea bomba
hasa ukichukulia na uwepo wa Wema Sepetu ndani yake ... ...Bado
msisitizo wa wasanii wakubwa kukubali kutungiwa nyimbo unawekwa ili
kupata ladha tofauti ...Je wewe una maoni gani??