Meneja
chapa wa bia ya Serengeti Premium, Bw.Rugambo Rodney (wa pili kulia),
akionyesha namba ya simu ya mshindi wa mwisho wa shindano la Tutoke na
Serengeti, ambapo Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe, Tanga aliibuka
mshindi.Msimamizi toka PWC, Golder Kamuzora na (wa pili kulia), Afisa
mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha,Bw. Jehud Ngolo (wa
kwanza kushoto) Afisa Mauzo toka SBL, Anitha Moshi, (wa kwanza kulia).
Droo hiyo iliyofanyika katika baa ya Hongera jijini Dar es salaam.
Mmoja
wa washiriki wa droo ya mwisho ya “Tutoke na Serengeti,” Morris Maro
wa pili toka kulia akibonyeza kitufe cha laptop kuchezesha droo hiyo
wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa mbugani” katika
kampeni ya Tutoke na Serengeti. Droo hiyo ilifanyika Hongera baa iliyopo
Kijitonyama jijini Dar es salaam amapo Bw. Robert Gabriel mkazi wa
Korogwe,Tanga aliibuka mshindi. Kwenye picha ni Meneja chapa bia ya
Serengeti premium Bw. Rugambo Rodney (wa pili kushoto), Afisa
mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Jehud Ngolo (wa kwanza
kushoto), na Getrud Mzava*mteja) aliyeitwa kushuhudia, droo hiyo
ikichezeshwa kwa haki ndani ya ukumbi wa Hongera baa-Kijitonyama jijini
Dar es salaam.
Mmoja
wa wateja wa Serengeti Premium Lager, Getrud Mzava ,akitaja namba za
simu za mshindi wa mwisho katika droo ya Tutoke na Serengeti wakati wa
kumtafuta mshindi wa mwisho wa Mtoko wa mbugani, ambapo mkazi wa
Korogwe,Tanga,Bw.Robert Gabriel aliibuka mshindi wa Mtoko wa Mbugani.
Droo hiyo ilichezeshwa ndani ya ukumbi wa Hongera-Kijitonyama jijini Dar
es Salaam.
Meneja
Bia chapa ya Serengeti Premium Lager, Bw. Rugambo Rodney (wa pili
kushoto), akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa mtoko wa mbugani, Bw.
Robert Gabriel mkazi wa Korogwe-Tanga, baada ya kuibuka mshindi wa
mwisho wa shindano la Tutoke na Serengeti katika droo iliyochezeshwa
ndani ya ukumbi wa Hongera baa-Kijitonyama jijini Dar es salaam.Kulia ni
Afisa mwandamizi toka Bodi ya michezo ya kubahatisha, Jehud Ngolo.
Meneja
chapa wa bia ya Serengeti Premium Bw. Rugambo Rodney, (kushoto)
akiongea kwa njia ya Simu na mshindi wa “Mtoko wa mbugani” Robert
Gabriel mkazi wa Korogwe-Tanga, baada ya kuibuka mshindi wa mwisho wa
shindano la Tutoke na Serengeti. Droo hiyo ilichezeshwa ndani ya ukumbi
wa Hongera Baa-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wasanii toka SBL wakikonga nyoyo za washiriki wa Droo ya Tutoke na
Serengeti wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa Mbugani”
ambapoBw.Robert Gabriel toka Korogwe-Tanga aliibuka mshindi wa droo hiyo
iliyochezeshwa jana katika Baa ya Hongera iliyopo Kijitonyama jijini
Dar es Salaam.
Mmoja
wa washindi wa shindano la Tutoke na Serengeti, Bw.Godfrey Mpiruka
aliyeibuka na zawadi ya Limo Bajaji siku za nyuma akiteta jambo na afisa
toka SBL wakati wa kuchezeshwa kwa droo ya mwisho ya shindano hilo,
lililofanyika katika baa ya Hongera iliyopo-Kijitonyama jijini Dar es
salaam.
Droo
ya mwisho ya kampeni ya Tutoke na Serengeti imemshuhudia mkazi wa
Korogwe Tanga Bw. Robert Gabriel Moriale akitangazwa mshindi katika
fainali ya kampeni “Tutoke na Serengeti”. Fainali hiyo imefanyika katika
ukumbi wa Baa ya Hongera iliyopo maeneo ya Kijitonyama-Dar es salaam
karibu na chuo cha Ustawi wa jamii.
Mshindi
huyo alijipatia fursa ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti
ambapo ataongozana na mtu wake yeyote wa karibu kwa muda wa siku tatu
huku SBL kupitia bia yake ya Serengeti Premium ndio itahusika kugharamia
usafiri, chakula, malazi sambamba na fedha taslim za mshindi kujikimu
pindi atakapokua safarini.
Akiongea
kupitia njia ya simu mara baada ya kutangazwa mshindi wa mtoko wa
mbugani, Bw.Robert (49)alipokea taarifa hizo kwa furaha na alisikika
akishangilia kwa kelele baada ya kuambiwa kwamba amejishindia “Mtoko wa
Mbugani”.
Alipoulizwa
kama alishawahi kushinda chochote kabla ya zawadi hiyo, Robert alijibu
“Nimekuwa nikishiriki tangu mwanzo na nimepata bia za bure nyingi tu
pamoja na pungozo la Tsh 300. Lakini hii ya leo kwa kweli sikuitarajia
kabisa”
Akiongea
wakati wa kufunga kampeni hiyo, Meneja chapa wa bia ya Serengeti
Premium Lager , Bwana Rugambo Rodney alisema, “Tumefurahishwa sana na
ushindi wa bwana Robert na tunapenda kumshukuru kwa kushiriki na
tunaamini aliifurahia bia ya Serengeti Premium ambayo imemletea furaha
ya kipekee siku ya leo.
Rodney
pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru washiriki wote kwa kutumia muda wao
wa thamani katika promosheni hii na kuwapa moyo wale ambao
hawakubahatika kushinda mtoko wa mbugani, Bajaj au bia za bure kutokata
tamaa na kushiriki tena nyakati zijazo kwani SBL imekuwa mstari wa mbele
katika kurudisha kiasi cha faida waliyopata kwa wateja wake. Aliongeza
kuwa wateja wakae mkao wa kula kwani kuna kitu kikubwa kinaandaliwa kwa
ajili yao.
Wakati
kampeni hii iliyodumu takribani miezi minne inafikia tamati, SBL imetoa
shukrani za pekee kwa wateja wake wa Serengeti Premium Lager baada ya
kushuhudia washiriki zaidi ya milioni moja wakijaribu bahati zao na
kuifanya promosheni ya “Tutoke na Serengeti” kuwa yenye mafanikio
kutokana na muitikio mkubwa na uelewa kutoka kwa wananchi.
Kampeni
imewazawadia wateja mbalimbali fursa ya kutembelea mbuga ya wanyama ya
Serengeti wakati wengine wakiondoka na zawadi murua kama vile Limo Bajaj
ambazo kwa kiasi kikubwa zitabadilisha maisha yao. Kulikuwa pia na
fedha taslim za kila wiki, bia za bure, na punguzo la Tshs300 katika
kila bia ya Serengeti Premium.
Promosheni hii ya nchi nzima pia ilipata ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa B-Pesa, wataalamu wa
teknolojia mpya ya usambazaji fedha waliochangia Limo Bajaj sita kwa
washindi mbalimbali. Pia walihusika na usambazaji wa fedha kwa washindi
nchi nzima katika kipindi chote cha miezi mine ya kampeni.