“Wakati wa sakata la Escrow bungeni, kuna mjumbe mmoja wa PAC aliitwa na
vinara wa watuhumiwa wa Escrow na kutakiwa kusema uongo bungeni kuhusu
mimi kwa ahadi ya kupewa donge nono, mjumbe huyo alikataa, na hapo ndipo
vinara hao wa Escrow wakaapa kutenga Shilingi Milion 500 kwa kila jimbo
la kila mjumbe wa PAC kuhakikisha kuwa wajumbe hao wote hawarudi
bungeni.
Kwahiyo nahisi kuwa hiki kilichonitokea sasa ni sehemu ya mkakati huo maana sakata la escrow limegusa wengi, hadi majaji wamo.”
“Kama Katiba ingebadilishwa kabla ya uchaguzi mkuu 2015 na ikaruhusu
mgombea urais mwenye umri chini ya miaka 40, ningegombea urais, nahitaji
kuongoza nchi, kwa ubunge imetosha, lakini kwa kuwa haiwezekani,
nitagombea ubunge lakini si Kigoma Kaskazini, nitatafuta jimbo linguine
la kugombea ili nao nikawatumikie, Kigoma Kaskazini nimeshafanya kila
kitu, sitakuwa na jipya”
Hajasema atagombea kupitia chama gani,
Je, wewe ungependa agombee kwa chama gani, jimbo gani na nini maoni yako kuhusu kauli hii?