BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???

Odama Bongo Movies akiwa na Mtoto wake
Kupata mimba ni jambo la heri na heshima kwa mwanamke. Mwanamke anaposhika mimba hujiona amekamilika lakini yule ambaye siku zinakwenda lakini kila akitega hanasi, hujisikia vibaya.

Hata hivyo, suala la ujauzito limekuwa likipokewa kwa hisia tofauti na mastaa wa Bongo. Wapo ambao wakipata mimba, dunia nzima itajua. Watajipiga picha na kuzitundika mtandaoni huku kila sehemu zenye mikusanyiko wakijiachia.

Lakini wapo ambao wakinasa, hata shughuli zao zinasimama. Hutawaona mtaani, wakiulizwa kama wana mimba wanakataa.Ni kweli wataficha mimba hadi wanakuja kujifungua. Hawa tunawaita mahodari wa kuficha ujauzito. Wafuatao ni wale waliotia fora katika siku za hivi karibuni kwa kuficha ‘vitumbo’ vyao.

Snura Mushi
Utakumbuka jinsi alivyojificha mara baada ya kunasa mimba ya huyo mtoto mchanga aliyenaye sasa. Hata pale alipojifungua, alikuwa mgumu kukubali kuwa amezaa.

Halima Yahaya ‘Davina’
Huyu ni mke wa mtu lakini naye alipobeba mimba ya mtoto wake wa pili, alificha ujauzito wake na hakuonekana sehemu yoyote hadi alipojifungua.

Husna Sajent
Yapo madai kuwa mwanadada huyu ana mimba ya msanii mwenzake (jina kapuni kwa sasa). Mwenyewe akipigiwa simu kuulizwa anakataa na sasa hivi haonekani kwenye minuso kama ilivyokuwa kawaida yake.

Odama
Muite Jennifer Kyaka. Mwanaye wa kiume aliyenaye alificha sana ujauzito wake. Kuna wakati alinaswa kwenye harusi ya mdogo wake akaulizwa lakini alikataa, hakuonekana tena mpaka alipojifungua.

Maimartha Jesse
Ni mke wa jamaa aitwaye Shaa. Huyu naye wengi walimshangaa kuficha mimba yake wakati alikuwa ndani ya ndoa, hata hivyo alisema aliamua tu, na kweli picha ya ujauzito wake haikuweza kupatikana kirahisi.

Queen Suzy
Bwana wake ni mwanamuziki aitwaye G-Seven. Naye alificha sana mimba yake, picha yake ilikuwa adimu na hakuweza kusikika kabisa mpaka pale zilipovuja kuwa amepata mtoto wa kike

Welu Sengo
Ana mpenzi wake lakini hajulikani. Wakati ni mjamzito, alipotea kabisa! Zikavuja kuwa ana mimba akakataa. Akasakwa sana ili picha ipatikane lakini mapaparazi wakaambulia patupu.

Safina
Ni staa wa igizo la Mizengwe, jina lake kamili ni Jesica Kindole. Ulishawahi kuona kitumbo cha mtoto wake wa kiume aliyenaye sasa? Jibu litakuwa hapana!

Salma Salmini- Sandra
Huyu naye ni muda mrefu zimevuja kuwa ni mjamzito lakini mpaka leo hii hakuna ushahidi na inasemekana anajificha kweli.Hao ni baadhi ya mastaa wa kike ambao katika siku za hivi karibuni walipata mimba lakini wakajificha.

GPL