Meneja wa Bia chapa Serengeti Primium Lager, Rugambo Rodney, (katikati) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa sita wa Limo Bajaji, Ramadhani Abubakar, katika shindano la “Tutoke na Serengeti” lililofanyika jana makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Baraka Majid na kushoto ni msimamizi toka PriceWater Cooper, Golder Kamuzora
Meneja wa Bia chapa Serengeti Premium Lager, Rugambo Rodney, (katikati) akibonyeza kitufe wakati wa kutafuta mshindi wa sita wa Limo Bajaji, katika shindano la “Tutoke na Serengeti” lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Kulia ni msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Baraka Majid na kushto ni msimamizi toka PriceWater Cooper, Golder Kamuzora.
SERENGETI
BREWERIES LTD
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
MKAZI WA MWANZA ASHINDA BAJAJI YA SITA YA PROMOSHENI
YA TUTOKE NA SERENGETI
Bajaji ya sita ya kampeni ya Tutoke na Serengeti,
safari hii itaelekea mkoani Mwanza baada ya bwana. Ramadhan Abubakar
kutangazwa kuwa mshindi wa Limo Bajaj, kufuatia ushiriki wake yakinifu
tangu kuanza kwa kampeni hii.
Akiongea kwa njia ya simu, Abubakar (28) ambaye
ni fundi umeme na mkazi wa Nyamagana, Mwanza alielezea furaha yake baada
ya kuelezwa na SBL kwamba ameshinda Limo Bajaj mpya katika kampeni ya
Tutoke na Serengeti…. “Aisee Mungu ni Mwema,…alitahamaki,… asante
sana kwa kunipa habari hii njema sikutarajia kushinda kabisa.”
Baada kuulizwa ni kwa namna gani ataitumia bajaji
aliyoshinda katika shughuli zake za kila siku , alisema ataitumia Bajaji
hii kwa shughuli za usafirishaji. Mwakazi aliongeza kwamba bajaji hiyo
itamsaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato cha familia kwa zaidi ya
asilimia 50 huku akiwa na lengo la kujiendeleza kitaaluma kwenye ufundi
umeme.
Akiongea na vyombo ya habari leo katika makao makuu
ya SBL yaliyoko Chang’ombe Dar es salaam, Meneja chapa wa Serengeti
Premium Lager Mr. Rugambo Rodney alisema “ Mshindi wetu wa sita wa
Limo Bajaj nae anatoka nje ya Dar es salaam kuashiria kwamba kampeni
hii imepokelewa vizuri mikoani kinyume na ilivyozoeleka na watu
wengi kwamba kampeni za namna hii ni za wakazi wa Dar tu. Rodney
aliongeza kuwa kwa sasa imebaki nafasi moja ambayo ni ya Mtoko wa mbugani
huku akiwahimiza wateja kutumia mwezi huu wa wapendanao kuwa “Surprise”
na kutoa zawadi ya “Mtoko wa mbugani kwa wenza wao ndani ya hifadhi
ya taifa ya Serengeti.
Kwa upande mwingine ujumbe kutoka BPESA wataalam
wa teknolojia ambao katika promosheni hii wanahusika na usambazaji wa
fedha kwa washindi kupitia njia ya simu maeneo
mbalimbali hapa nchini, imethibitisha kuwalipa fedha taslim washindi
wa kila wiki.
Ili kushiriki katika promosheni hii, mteja anatakiwa
awe na umri wa miaka 18, anunue Serengeti Premium Lager na aangalie
chini ya kizibo ambapo atakutana na namba maalum anazotakiwa kuzituma
kwa njia ya sms kwenda 15317.
Kadiri unavyoshiriki mara nyingi ndivyo unavyojiweka katika nafasi ya
ushindi.