Irene Uwoya amesema ingawa Jaguar alishindwa kuja kuzungumza na
wazazi wake kuhusu ndoa yao, bado wanawasiliana vizuri na kila kitu kipo
sawa.
Akizungumza na na chanzo makini leo Irene amesema mahusiano yake na Jaguar yapo japo hajafanya maamuzi ya kuolewa.
“Jaguar hakuja kuna vitu ambavyo vilitokea vikasababisha asije,”
amesema mrembo huyo. “Kila siku naongea naye na uamuzi wake upo pale
pale. Mimi mwenyewe bado sijafanya maamuzi ya kusema niolewe lakini
akija ndo tutaongea kila kitu.”
Haya hivyo Irene amesema hawezi kuzungumzia ndoa yake na mcheza soka
wa Rwanda, Ndikumana waliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Krish.
“Sasa kuhusu hilo nisingependa kuliongelea, mimi nadhani sijui hata nisemeje, sipendi kuongelea mambo yangu binafsi.”