
Meneja
Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija
(wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la
“Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na
utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea
maendeleo binafsi. (katikati) ni Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za
Diageo-Serengeti Breweries Limited (SBL), Stanley Samtu na kulia ni Dj
maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.

Dj maarufu
kutoka Ireland Frank Jez (wa kwanza kulia) akitoa historia yake fupi ya
maisha jinsi alivyofanikiwa kwa kuipenda kazi yake na kuifanya kwa
furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa
jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa
na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika
kujiletea maendeleo binafsi. (Katikati) niMkuu wa masoko bidhaa za pombe
kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited(SBL) Stanley Samtu na
(kulia) ni Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti
(SBL) Shomari Shija. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.

Meneja
Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija
(wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la
“Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na
utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea
maendeleo binafsi. (katikati) ni Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za
Diageo-Serengeti Breweries Limited (SBL), Stanley Samtu na kulia ni Dj
maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.

Mkuu wa
masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited (SBL),
Stanley Samtu(kushoto), Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya
Serengeti (SBL) Shomari Shija (kulia) na Dj maarufu kutoka Ireland Frank
Jez (katikati) wakionyesha bidhaa mbalimbali za Johnnie Walker wakati
wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha
itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa
kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo
binafsi. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.
Chapa
maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
Breweries “Johnnie Walker” imezindua kampeni mpya iliyopewa jina la
“Furaha itakufikisha mbali” siku ya leo katika hoteli ya Serena jijini
Dar es salaam ikiwa na lengo la kuwahamasisha watu kuwa na furaha katika
kila wanachokifanya kwa vile furaha huleta maendeleo na sio kinyume
chake kama wengi wanavyodhani.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa Kampeni hiyo katika hoteli ya
Serena, Mkuu wa kitengo cha Masoko pombe kali wa Kampuni ya bia ya
Serngeti (SBL) Stanley Samtu alisema “Kama chapa, Johnnie Walker
imesimama daima kwenye upande wa maendeleo. Imekuwa hivyo kwa miaka
takribani 200 tangu mwanzilishi Johnnie Walker alipoanza ufundi wake.
Uzoefu umetufundisha kwamba maendeleo hayatakiwi kuwa safari ya kupanda
tu na isiyo na kikomo bali tunaweza kupiga hatua na kufurahia katika
malengo tunayoweza kuyafikia kila kukicha. Hiyo ndio maana halisi ya
kampeni hii ya Furaha itakufikisha mbali zaidi”.
Kufurahia
kile unachokifanya ni sehemu kubwa na muhimu ya kufanikiwa na kuwa na
maendeleo. Katika juhudi za kufikisha ujumbe kwa wahusika, Johnnie
Walker inategemea kuwamulikia baadhi ya nyota katika fani mbalimbali
waliojizolea umaarufu kutokana na mafanikio walioyafikia. Hawa ni pamoja
na Sheria Ngowi wa tasnia ya mitindo, Dj Frank Jez kutoka Ireland na Dj
Peter Mo. Vijana hawa wote wamebobea katika kile wanachokifanya na
wamekuwa mfano wa kuigwa nchini. Wamekuwa sehemu ya dunia ya watu ambao
wanaaamini kuwa chanya siku zote katika kazi ni moja kati ya vitu
viliyowasaidia kufika mbele zaidi katika fani zao.