Meneja mipango ya biashara, matukio na uhamasishaji wote wa kampuni ya Serengeti Breweries Limited
Bw. Denis Tairo akizungumza na wateja wa bia ya Serengeti Premium Lager wakati
wa uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection
kwa wakazi wa kanda ya ziwa jijini Mwanza ambapo bia ya Serengeti Premium Lager
ya SBL imetuzwa medali tatu za dhahabu kutoka kwenye viwanda vyake vyote
vitatu; cha Dar es salaam, Mwanza na Moshi kwa mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika
katika baa ya “The dreams” iliyopo Kona ya Bwiru jijini Mwanza.
Mdau wa bia ya Serengeti Premium Lager Ben Rockman akijaribu kuitambua bia ya
Serengeti Premium Lager ,aliposhiriki kwenye shindano la kumtafuta “Serengeti
Masta” wa baa ya “The dreams” ya jijini Mwanza wakati wa kusherekea uzinduzi kampeni
ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo kwa mwaka huu
bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL imejinyakulia medali tatu za dhahabu
kutokana na ubora wake. Kauli mbiu ya kampeni hii ikiwa ni “SERENGETI PREMIUM
LAGER. TUNAIJUA BIA NA HII NDIO YENYEWE”.
Wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Brewieries Limited wakiwa na Mabalozi wa
kinywaji hicho wakati wa kutambulisha Tuzo ya Dhahabu ya Monde inayotambulika
kimataifa baada ya bia ya Serengeti Premium Lager kukidhi viwango vya juu vya
ubora katika hafla iliyofanyika katika Baa ya Oriental ,Majengo mjini Moshi
mwishoni mwa wiki.
Mkazi wa Kona ya Bwiru jijini Mwanza Bw. Godfrey Urio akishiriki katika shindano
la kumpata “Serengeti Masta” ambapo mpenzi wa kinywaji hicho anatakiwa aitambue
bia ya Serengeti Premium lager na kushiriki maswali ili kushinda. Shindano hilo
lilifanyika wakati wa kusherekea uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora
wa thamani ya Monde Selection kwa wakazi wa kanda ya ziwa jijini Mwanza ambapo
kwa mwaka huu bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL imejinyakulia medali tatu
za dhahabu kutokana na ubora wake. Shindano hilo litafanyika Tanzania nzima na
kuibua Mshindi mmoja kwa kila kanda na mwisho kumuibua wa kitaifa. Kauli mbiu
ya kampeni hii ikiwa ni “TUNAIJUA BIA NA SERENGETI PREMIUM LAGER NDIO YENYEWE”.