Diamond Platinumz kupitia akaunti yake ya Instagram amepost kuwa miongoni mwa ngoma anazopenda kusikiliza kwa sasa kwenye gari lake ni ile kolabo aliyofanya na Raymond ambayo hata hivyo amegoma kuitaja ni ngoma gani. Lakini kwa post hiyo inaonyesha kuwa wawili hao wanaowakilisha lebo ya Wasafi Classic wanaandaa ngoma ambayo wataitoa hivi karibuni ambapo mashabiki wake wanaonekana kuisubiri kwa hamu wakitaka Diamond aiachie.

kolabo
Post hiyo kama inavyoonekana kwenye ukurasa wa Instagram wa Diamond.
Raymond a.k.a RayVanny kwasasa bado anatamba na kibao cha Natafuta Kiki ambacho amekiachia hivi karibuni baada ya kufanya vizuri kwa ile ngoma yake iliyomtambulisha kwenye game inayojulikana kwa jina la ‘Kwetu’

Usipocheka kwa kuangalia video hii ya Masanja, nidai 10,000


 
Top