BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???

Msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ujio wake jijini Mbeya na mtazamo wake kwa akina dada juu ya uzazi wa mpango mara baada ya kumaliza kutumbuiza katika Tamasha lililopewa jina la “Divas Only Concert” ambalo lilifanyika jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Msanii Vanessa Mdee akifurahia jambo na mashabiki wake katika Tamasha la “Divas Only Concert” lililofanyika katika ukumbi wa Mtenda Sunset-Soweto jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. Msanii huyo aliporomosha burudani ya nguvu kwa madiva lukuki waliofika kushuhudia tamasha hilo ambalo lililoandaliwa na chapa ya TRUST toka shirika lisilola kiserikali la DKT lengo la Tamasha likiwa ni kuwahamasiha kuamka kifikra na kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wasichana na kina mama wa jiji hilo.
Msanii Vanessa Mdee (katikati) akiwa pamoja na wanenguaji wake katika Tamasha la “Divas Only Concert” lililofanyika katika ukumbi wa Mtenda Sunset-Soweto jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. Msanii huyo aliporomosha burudani ya nguvu kwa madiva lukuki waliofika kushuhudia tamasha hilo ambalo lililoandaliwa na chapa ya TRUST toka shirika lisilokua la kiserikali la DKT lengo la Tamasha likiwa ni kuwahamasiha kuamka kifikra na kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wasichana na kina mama wa jiji hilo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee akiimba katikati ya mashabiki wake wakati wa Tamasha la “Divas Only Concert” lililoandaliwa na chapa ya Trust toka DKT International ambalo lilifanyika jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.
---
TRUST imeendelea kuzikonga nyoyo za mashabiki wake hususani wakina dada katika mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya “Divas Only” ambapo kwa wikiendi hii ilikua ni zamu ya jiji la Mbeya baada ya Tamasha hilo kuzinduliwa rasmi jijini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kama ilivyo ada Tamasha hilo humshirikisha Diva wa nguvu na msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee ambaye alizikonga nyoyo za mashabiki wake vilivyo. Tamasha hilo liliwavutia madiva kibao kutoka maeneo ya karibu pamoja na vyuo mbalimbali vya jijini Mbeya kama TECU, Mzumbe, CBE na TIA ambapo kiingilio cha Tamasha hilo kilipangwa kuwa Tsh. 10,000/= tu.

Trust ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa kwa ajili ya wanawake. Trust ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye.

Madiva wa Trust wanataka kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili ya mafanikio; Trust ipo hapa kukusaidia wakati wa safari hii. “Kwa mara nyingine ilikuwa ni fursa nzuri ya kufurahi kwa muda tuliopata wa kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa jijini Mbeya na kufurahi na kuelimishana, tumejifunza kutoka kwa wataalamu mambo mengi na njia nyingi bora, kwamfano njia ya Kitanzi ni bora sana ina ufanisi wa zaidi ya asilimia 99.9 na pia ni bora sana kwakua aina nyingi hazina vichocheo ”…alisema Sialouise Shayo Meneja Masoko Trust.

Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, njoo ukutane na Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika Tamasha letu lingine jijini Mwanza Desemba 13, Malaika Beach Resort. Huwezi kufika? Tutafute kupitia ofisi zetu zinazopatikana Dodoma, Mbeya na Mwanza au kwa kupitia tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!