Mbunge wa viti Maalum Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia UVCCM Mkoa wa Kigoma, Zainab Katimba (aliyevaa Gum Boots), akiwaongoza Vijana wenzake katika zoezi la kufanya usafi, ambapo wamefanya usafi katika eneo la Hospitali ya Maweni. |
UMOJA
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kigoma wakiongozwa na Mbunge
wa Vijana Mh. Zainab Katimba wameunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa kufanya usafi katika
hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kigoma Maweni.
Usafi
huo ambao umeenda sambamba na kugawa zawadi mbali mbali kwa wagonjwa hospitalini
hapo, ambazo ni sabuni na vifaa mbali mbali vya usafi juisi na biskuti umelenga
kuunga mkono zoezi la kufanya usafi katika siku ya maadhimisho ya siku ya
Uhuru.
Akizungumza
hospitalini hapo Bi. Katimba alisema kuwa, wao kama vijana wameamua kuwa mfano
kwa kuanza kutekeleza agizo hilo kwa kufanya usafi hospitalini hapo, Soko la
Mwanga lililopo mjini Kigoma pamoja na kutembelea kituo cha watoto yatima
ambapo wamefanya usafi kituoni hapo na kugawa zawadi mbalimbali kwa watoto
ikiwemo vyakula.
Alisema
lengo la kufanya usafi ni kuhakikisha magonjwa mbali mbali kama kipindupindu yanatokomezwa
kwa kuweka maeneo yote kuwa safi. "Leo tumeamua kuanza na hili zoezi
rasmi, lakini zoezi hili ni endelevu" Katimba alisema.
Aidha
Mhe. Katimba alitoa wito kwa vijana wote tanzania nzima wajikite kuunga mkono
jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha maisha ya
watanzania. Mhe. Katimba ametoa agizo kwa vijana wote Tanzania nzima kuwa
mstari wa mbele katika kufanya usafi siku ya tarehe 9 Dec 2015.