BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???

Baadhi ya madiva wa jiji la Mwanza wakiwa kwenye pozi la Red Carpet wakati wa Tamasha la “Trust Divas Only” ambalo lilifanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya akina dada na ni mahususi kwa ajili ya utoaji elimu ya afya ya uzazi na maendeleo yao ya baadae.

Madiva mbalimbali wakijiandikisha wakati wa ufunguzi wa Tamasha la “Divas Only”ambalo lilikuwa maalum kwa ajili ya kuwaelimisha akina dada juu ya afya ya uzazi na maendeleo yao ya baadae. Tamasha hilo ambalo lilipambwa vilivyo na burudani toka kwa Msanii Vanessa Mdee lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza.Moja ya Madiva wa jiji la Mwanza akiimba accapela kwenye tamasha la “Trust Divas only” lilofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza katika Ukumbi wa Malaika Beach Resort. Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya akina dada ambalo lilitoa elimu ya afya ya uzazi kwa madiva wa jiji hilo.


Msanii wa Bongo fleva Vanessa Mdee akitumbuiza kwenye Tamasha la “Trust Divas Only” lililofanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya kina dada na limekua likitoa elimu juu ya afya ya uzazi na maendeleo ya baadae ya madiva hao tokea uzinduzi wa mfululizo wa matamasha hayo jijini Dodoma wiki mbili zilizopita.Msanii wa Bongo fleva Vanessa Mdee, akipiga picha na baadhi ya mashabiki wake wakati wa Tamasha la “Divas only” ambalo ni mahusisi kwa ajili ya kuwaelimisha madiva mbalimbali kuhusu elimu ya afya ya uzazi. Tamasha hilo la mwisho lilifanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza baada ya kuzunguka katika majiji ya Dodoma na Mbeya katika wiki zilizopita.

Mwanza
Tamasha la “Trust Divas only” limefunga pazia lake rasmi usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Malaika Beach resort uliopo pembezoni mwa ziwa Victoria jijini Mwanza. Wakazi na madiva wa mkoa huo walijitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha hilo la mwisho na la aina yake lakini kikubwa zaidi kupata elimu na hamasa juu ya uzazi wa mpango na mambo yanayowahusu wakina dada katika kupanga maendeleo yao ya baadae.
Aliyelipamba Tamasha hilo si mwingine bali ni diva wa nguvu na msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee ambaye tokea awali amekua akishirikiana na Trust katika mfululizo wa matamasha hayo yaliyoanza rasmi wiki mbili zilizopita jijini Dodoma.
Mara baada ya kupanda jukwaani na kuporomosha burudani ya nguvu Vanessa alionekana kushangiliwa kila kona na madiva hao waliokuwa wakiimba sambamba na msanii huyo ambae alifanikiwa kukata kiu ya madiva wengi wa mkoa huo waliojitokeza kwa wingi kushuhudia burudani yake.
Mfululizo wa matamasha hayo ya Trust ambayo ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa kwa ajili ya wanawake yamefikia tamati baada ya kuzunguka kwa muda wa wiki tatu kwenye miji mitatu tofauti ili kuhamasisha madiva mbalimbali wajipange kwa ajili ya mafanikio yao ya baadae. Trust ipo katika kumsaidia diva wakati wote wa safari hii.
“Ni furaha yangu kubwa kuwa tumeweza kukamilisha zoezi hili kwa ufanisi mkubwa tangu tulipozindua matamasha haya jijini Dodoma”… alisema Meneja Masoko wa Trust Sialouise Shayo.
Bi. Shayo aliongeza kuwa katika zoezi zima wamefanikiwa kuwafikia madiva lukuki katika mikoa yote mitatu waliyoitembelea ambapo kwa pamoja wameweza kufurahi, kuelimishana na kujifunza kutoka kwa wataalamu mambo mbalimbali zikiwemo njia nyingi bora za uzazi wa mpango kama njia ya kitanzi ambayo ni bora sana  na ina ufanisi wa zaidi ya asilimia 99.9.
Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, Tutafute kupitia ofisi zetu zinazopatikana Dodoma, Mbeya na Mwanza au kwa kupitia tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo.