Mkuu
wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara (Kushoto) akipokea zawadi
ya wiski ya Johnnie Walker (Platinum Label) iliyotolewa na Kampuni ya
bia ya Serengeti katika kuthamini mchango wake kimichezo kwa kuasisi
uwanja wa gofu wa Lugalo. Anayekabidhi zawadi hiyo ni balozi wa pombe
kali ya Johnnie Walker Winfrida Kimario.
Mshindi
wa michuano ya gofu ya Waitara kwa wachezaji wakongwe wanawake
Priscilla Karobia (Katikati) akikabidhiwa zawadi yake baada ya kuwapiku
wenzake kwa mikwaju 82. Akikabidhi zawadi hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa
bodi ya (NIC) Dk. Edmund Mndolwa. Michuano hiyo hudhaminiwa na Kampuni
ya bia ya Serengeti ambayo hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni
ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali
George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.
Mkuu
wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara (Kushoto) akipokea tuzo
iliyotolewa na Uongozi wa klabu ya gofu ya Lugalo katika kuthamini
mchango wake kimichezo kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo. Michuano
hiyo hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti na hufanyika mara moja
kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa
Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa
Lugalo golf club.
Jaji
Mstaafu Mhe. Mark Bomani akipokea tuzo iliyotolewa na Uongozi wa klabu
ya gofu ya Lugalo kwa kuthamini mchango wake katika mchezo wa gofu hapa
nchini. Michuano ya gofu ya Waitara hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya
Serengeti na hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi
mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George
Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.
Meneja
Chapa wa pombe kali wa Kampuni ya bia ya Serengeti Shomari Shija
(Kushoto) akipokea tuzo iliyotolewa na uongozi wa klabu ya gofu ya
Lugalo kwa kuthamini mchango wa Kampuni hiyo kwa kudhamini michuano ya
gofu ya Waitara kila mwaka. Michuano hiyo hufanyika mara moja kila mwaka
kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi
(Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo
golf club.
Mshindi
wa jumla wa michuano ya gofu ya Waitara George Nyakundi (katikati)
akiwa na nyuso ya furaha baada ya kutangazwa rasmi kama mshindi wa jumla
wa michuano hiyo ambapo alikabidhiwa kikombe pamoja na zawadi
mbalimbali. (wa pili kushoto) ni Mgeni ramsi wa michuano hiyo Jaji
(Mstaafu) Mark Bomani na (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa majeshi
(Mstaafu) George Waitara na wa kwanza kulia ni Meneja chapa wa pombe
kali wa Kampuni ya bia ya Serengeti Shomari Shija. Michuano ya gofu ya
Waitara hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti na hufanyika mara
moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa
Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa
Lugalo golf club.
--
Michuano
ya gofu ya Waitara yanayodhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
kupitia pombe yake kali ya Jonnie Walker imefana na kumalizika vizuri
siku ya jumamosi ambapo MCHEZAJI George Nyakundi ameibuka mshindi wa
jumla wa mashindano ya kila mwaka ya Kombe la Waitara yalilofanyika
kwenye Viwanja vya gofu vya Klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es Salaam.
Nyakundi
anayecheza katika kiwango cha ubora wa mchezo wa gofu (handicap) 22
alionesha kiwango cha juu zaidi katika mashindano hayo kwa kupiga
mikwaju nett 65 na kuwashinda wachezaji zaidi ya 118 waliokuwa wakiwania
Kombe hilo.
Nafasi ya pili ya jumla ilikwenda kwa Michael Obare ambaye alichuana vikali na mshindi akirejea na mikwaju nett 66.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliofika katika viwanja hivyo, Meneja Chapa wa
pombe kali wa kampuni ya bia ya Serengeti Shomari Shija alisema kuwa
wamedhamini mashindano hayo kwa mara ya tano sasa ili kuendelea kuenzi
heshima ya muasisi wa klabu hiyo Jenerali Mstaafu George Waitara.
Akitangaza
matokeo ya washindi mbalimbali katika makundi tofauti Kapteni wa klabu
ya gofu Lugalo Japhet Masai alisema katika kundi la wachezaji wa viwango
vya Daraja A ambao ni wa kiwango cha juu katika mchezo huo mchezaji
chipukizi Suleiman Kessy mwenye handicap 9 alishinda kwa kupiga mikwaju
nett 69, Jumanne Ally handicap 8 alishika nafasi ya pili akiwa na
mikwaju 70, wakati Juma Likuli mwenye handicap 8 alimaliza nafasi ya
tatu akiwa na mikwaju 70 pia.
Mchezaji
Nicolaus Chatanda handicap 11 alishinda kombe kwa wachezaji wa Daraja B
akiwa na mikwaju 68, akifuatiwa na nahodha wa Klabu ya Gymkhana Dar es
Salaam, Akhil Yusufali handicap 16 akiwa na mikwaju 71 na Priscus Nyoni
handicap 12 alishika nafasi ya tatu akiwa na mikwaju 72.
Kelvin
Manuhwa handicap 19 alishinda kwa kundi la wachezaji wa Daraja C akiwa
na mikwaju 72 na kufuatiwa na R. Rwiguza handicap 24 aliyepiga 74.
Kundi
la wachezaji waandamizi wanaume kombe lilikwenda kwa Joseph Tairo
handicap 13 mikwaju 73, nafasi ya pili alikuwa Jenerali Mstaafu Mirisho
Sarakikya handicap 19 aliyepiga mikwaju 73 pia , wakati Edmund Mndolwa
handicap 9 alipiga mikwaju 74 na kumaliza nafasi ya tatu.
Pricilla
Karobia handicap 17 alishinda kwa upande wa wachezaji wakongwe wanawake
akiwa na mikwaju 82 na Lina Nkya handicap 15 alishika nafasi ya pili
baada ya kurejea na mikwaju 88.
Kwa
upande wa kundi la wanawake Tayana William handicap 24 aliibuka mshindi
kwa kupiga mikwaju 72, akifuatiwa na Vailet Peter handicap 13 akiwa na
mikwaju 74 na Vicky Elias handicap 13 alishika nafasi ya tatu baada ya
kurejea na mikwaju 76.
Mbali
na wachezaji wa ridhaa mashindano hayo pia yalihusisha kundi la
wachezaji wa kulipwa ambapo Geofrey Leverian alirejea na mikwaju 75
gross na kuibuka mshindi wa kundi hilo lililohusisha wachezaji 18.
Nafasi ya pili na tatu ilikwenda kwa mchezaji mkongwe Mbwana Juma na
Nuru Mollel waliopiga mikwaju 76 na 77.
Kwa
upande wake muasisi wa michuano hiyo Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali
George Waitara aliwashukuru washiriki wote kwa kuonyesha ni jinsi gani
wameendelea kuthamini michuano hiyo na kuwataka kuendelea na moyo huo.
Waitara
pia alitumia nafasi hiyo kuishukuru Kampuni ya bia ya Serengeti na
kumpongeza Mkurugenzi Mkuu (mstaafu) wa Kampuni hiyo Bw. Steve Ganon
ambaye mara zote hakusita kudhamini michuano hiyo na kuomba wadau
wengine kuiga mfano huo.
Naye
Mgeni rasmi wa michauano hiyo Jaji (Mstaafu) Mark Bomani alitoa
changamoto ya wadau wa mchezo huo kushiriki katika kuongeza viwanja
vingi zaidi vya mchezo huo huku akianisha maeneo kama Dodoma, Mwanza na
Mbeya ambapo wadau hao wanaweza kuendeleza mchezo huo.
Mashindano
ya gofu ya Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara huandaliwa
na kufanyika kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wake wa
kimichezo nchini kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club. Uwanja
huo ulianzishwa mwaka 2006 kwa mchango mkubwa uliotolewa na Jenerali
mstaafu George Waitara kipindi alichokuwapo madarakani, pia kuendelezwa
na Mkuu wa Majeshi aliyefuata na aliyeko madarakani kwa sasa Jenerali
Davis Mwamunyange.