Mkazi wa Arusha na mpenzi
wa bia ya Serengeti Premium Lager Laota Elias akishiriki katika shindano la
mwisho la kumtafuta Serengeti Masta wa jumla kwa mkoa wa Arusha katika
kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager. Mashindano hayo ya
mwisho yalifanyika katika baa ya Bondeni iliyopo Kijenge juu jijini Arusha
ambapo yaliwakutanisha washindi mbalimbali wa baa za mkoa huo waliofika
kuchuana vikali ili kumpata mshindi wa jumla. Kampeni hiyo imefikia tamati
jijini humo baada ya kudumu kwa takribani miezi miwili ikizunguka baa kwa baa
kusaka washindi waliopewa jina la “Serengeti Masta”.
Mkazi wa Arusha Cleophas John
akifurahi pamoja na marafiki zake baada ya kupita kwenye ngazi ya kwanza ya
shindano la kumtafuta “Serengeti Masta” wa mkoa wa Arusha linaloendeshwa na bia
ya Serengeti Premium Lager toka SBL wakati wa shindano hilo ambalo lilifanyika katika baa ya
Bondeni-Kijenge juu jijini Arusha. Shindano hilo limefikia tamati jijini humo
baada ya kudumu kwa takriban miezi miwili (2) ikiwaburudisha na kuwazawadia
wateja wa bia hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji
huduma kwa wateja
Mratibu wa mashindano ya
kumsaka Serengeti Masta Yassin Khalfan (katikati) akiwa na baadhi ya washiriki
wa shindano hilo kutoka Baa mbalimbali jijini Mbeya kushoto ni Faraji Mbwambo
kutoka Gambino Bar na Ibrahim Allan kutoka Liz Pub.
Kampeni hiyo ya Serengeti Masta imewakutanisha wateja na mameneja wa bia hiyo
katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia ya Serengeti Premium Lager ambapo
mameneja hao walitoa zawadi mbalimbali kwa washindi walioweza kuitambua ladha
halisi ya bia hiyo katika kipindi chote cha kampeni ambapo pia waliweza kuwafikia wahudumu wa baa zaidi ya 4000 katika miji
tofauti.
Mshiriki wa shindano la Serengeti Masta na mkazi wa Arusha Daniel Mwakasungule akionja
ladha tofauti za bia zilizo mbele ya meza yake ili kuitambua ladha halisi ya
bia ya Serengeti Premium Lager katika shindano la kumpata Serengeti Masta wa
mkoa wa Arusha ambalo lilifanyika katika Baa ya Bondeni, Kijenge juu jijini
Arusha mwishoni mwa wiki hii.
Mshindi wa jumla wa shindano Serengeti
Masta kwa jiji la Mbeya Faraji Mbwambo kutoka baa ya Gambino jijini Mbeya
akionesha kitita cha fedha sh. 100,000 alizotunukiwa baada kuibuka mshindi wa
jumla wa kuitambua ladha ya bia ya Serengeti Premium Lager kati ya vinywaji
vitano vinavyozalishwa na kampuni ya SBL. Kampeni
hiyo ya Serengeti Masta imewakutanisha wateja na mameneja wa bia hiyo katika
kujifunza kwa undani kuhusiana na bia hiyo ambapo mameneja hao walitoa zawadi
mbalimbali kwa washindi walioweza kuitambua ladha halisi ya bia hiyo katika
kipindi cha kampeni
Mmoja wa wateja na mnywaji maarufu wa
bia ya Serengeti Premium Lager Tuntufye Mwakaje maarufu kwa jina la “Tupac” akiburudika na bia hiyo wakati wa shindano la
kumsaka Serengeti Masta wa jumla kwa wakazi wa jiji la Mbeya lililofanyika kwenye baa ya Mbeya Pazuri.