BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???

Mshereheshaji wa shindano la Serengeti Premium Lager liliopewa jina la “Serengeti Masta” Richard Godwin akitoa maelekezo kwa washiriki wa shindano hilo la mwisho kwa wilaya ya Ilala lililofanyika mwishoni mwa wiki katika baa ya Havana Park iliyopo Segerea jijini Dar es salaam. Shindano la Serengeti Masta limedumu jijini Dar na mikoani kwa takriban muda wa miezi mitatu sasa na kuweza kuzifikia baa zaidi ya 200 ambapo zawadi mbalimbali kama fedha taslim, fulana na bia za bure zimekuwa zikitolewa katika kuwahamasisha wateja wa bia hiyo kuendelea kuwa pamoja.
Mshereheshaji na mratibu wa mashindano ya kumsaka Serengeti Masta Richard Godwin akionyesha kiasi cha fedha taslim zilizowaniwa na “Serengeti Masta” wa wilaya ya Ilala wakati wa mpambano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika baa ya Havana iliyopo Segerea jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo imefikia kikomo baada ya kuzunguka katika baa mbalimbali jijini na mikoani katika kuwasaka washindi waliotambua ladha halisi ya bia ya Serengeti ambapo pia ilifanikiwa kuwafikia wahudumu zaidi ya mia tano katika baa tofauti tofauti waliopewa somo la utoaji huduma kwa wateja.
Mmoja wa washiriki wa shindano la “Serengeti Masta” Godfrey Dickson akishiriki kuchanganya ladha tofauti za chapa za bia mbalimbali kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti wakati wa shindano la kumtafuta Serengeti Masta wa wilaya ya Ilala lililofanyika katika baa ya Havana Park iliyopo Segerea jijini Dar es salaam. Shindano la” Serengeti Masta” lilianzishwa mahususi kwa ajili ya kurudisha shukrani kwa wateja wa bia ya Serengeti Premium Lager mara baada ya bia hiyo kushinda kinyang’anyiro cha bia ya kimataifa yenye viwango bora katika tuzo za “monde selection” za mwaka huu.
Mkazi wa Segerea Raymond Sanga akishiriki kuchanganya ladha tofauti za bia mbalimbali kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti wakati wa shindano la kumtafuta Serengeti Masta wa wilaya ya Ilala lililofanyika mwishoni mwa wiki katika baa ya Havana Park iliyopo Segerea jijini Dar es salaam. Pamoja nae ni balozi wa bia hiyo Blessing Zakaria. Shindano la Serengeti Masta limefikia kikomo jijini Dar es salaam ambapo limefanikiwa kuwaibua washindi mbalimbali kutoka katika wilaya zake zote tatu.
Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta kwa wilaya ya Ilala Raymond Sanga akionyesha fedha taslim Tsh. 100,000/= alizopokea toka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Segerea Nicholaus Charles Mafundo wakati wa shindano la mwisho la kumtafuta “Serengeti Masta” wa jumla wa wilaya hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika baa ya Havana Park iliyopo Segerea jijini Dar es salaam.
---
Kampeni ya “Serengeti Masta” iliyokua ikiendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti chini ya udhamini wa bia yake namba moja ya Serengeti Premium Lager, imefikia kilele jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki baada ya kampeni hiyo kuzunguka kwa muda wa miezi mitatu katika miji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Morogoro.

Katika kufunga Kampeni hiyo kwa kishindo, kwa kushirikiana mameneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, walijipanga kuwafikia mashabiki wengi zaidi wa bia hiyo ambapo iliwalazimu kufanya shindano la “Serengeti Masta” katika baa tatu zilizopo jijini Dar es salaam kwa siku tofauti.

Sherehe hizo ambazo zilionekana kuwafurahisha mashabiki wengi wa bia ya Serengeti Premium Lager, ziliambatana na burudani ya mziki, zawadi za fedha taslim, fulana na bia za bure.

Baadhi ya baa za jijini Dar es Salaam, ambazo zilizochaguliwa kuimalizia promosheni hiyo ni pamoja na Kisuma iliyopo Temeke, Zambezi Ubungo na Havana Park ya Segerea.

Akiizungumzia promosheni hiyo mmoja wa wateja maarufu wa bia ya Serengeti Premium Lager aliyehudhuria shindano la “Serengeti Masta” katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam, Bw. Salehe Kitwana, aliipongeza Kampuni ya bia ya Serengeti na mameneja wa bia hiyo, kwa kuibua kampeni ambayo imeweza kuwahamasisha wahudumu wa baa mbalimbali jijini Dar es Salaam na mikoani katika utoaji huduma bora kwa wateja wa bia hiyo, sambamba na kuwazawadia fedha taslim washiriki mbalimbali walioweza kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti baada ya bia hiyo kushindanishwa na bia nyingine tano zinazotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).

“Promosheni kama hii inawaunganisha mashabiki na kuwafanya waipende bia yao zaidi na zaidi pia nadhani huu ni mfano wa kuigwa na bia nyingine zinaweza kujifunza mengi kutokana na promosheni kama hii”.alisema Bw. Salehe

Naye Meneja Masoko wa bia ya Serengeti Premium Lager Bi. Anitha Msangi alisema,”Kampeni hii imekuwa ikiendeshwa kwa muda wa miezi mitatu sasa na kuanza kupamba moto baada ya mashabiki kuipokea kwa mikono miwili na kuifanya kuwa maarufu.

Alisisitiza kuwa, shindano la “Serengeti Masta” ni moja kati ya kampeni kubwa ambazo zimeweza kufanikiwa kiutekelezaji kwa mwaka huu, ikiwa ni moja ya kazi kubwa zilizofanywa na Kampuni ya bia ya Serengeti.

Bi. Msangi pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wateja wote wa bia ya Serengeti Premium Lager mameneja wa baa mbalimbali walioshiriki kwenye kampeni hii na wafanyakazi wote wa SBL nchi nzima kwa kuwaunga mkono na kushiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi zima la kampeni hiyo.

Aliongeza kuwa pamoja na ushiriki wa wateja kuwa mzuri lakini pia wamefanikiwa kuongeza mauzo ya bia ya Serengeti kufikia kiwango kikubwa kuliko hapo awali kwa mwaka huu.

Tafiti mbalimbali zilizofanywa na SBL katika kipindi cha miezi mitatu ya kampeni hii imedhihirisha kuwa kampeni hiyo haikufaidisha tu kampuni ya bia ya Serengeti bali pia baa zaidi ya 4000 zilizotembelewa na shindano hilo nchi nzima katika kipindi chote cha miezi mitatu.

Vilevile kampeni hiyo imeibua washindi mbalimbali waliopewa cheo cha Serengeti Masta ambao walijizolea fedha taslim na bia za bure, fulana na zawadi mbalimbali.

“Namshukuru Mungu na sisi pia tumebahatika kuweza kuwa sehemu ya kampeni hii kabla ya kufikia tamati na ninajiona kama mwenye bahati sana” alisema Meneja wa baa ya Kisuma Thomas Kimaro ambaye alihojiwa na waandishi wa habari wakati wa shindano la mwisho la Serengeti Masta lililofanyika kwenye baa yake.

Kimaro aliipongeza Kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwa mashuhuri wa kubuni mambo mapya kila kukicha na kuwasihi kuendelea kuleta promosheni kama hizi kwa kuwa zinaongeza mauzo ya bia hizo kwenye baa zao.

Kampeni ya Serengeti Masta ilianzishwa mahususi kwa ajili ya kurudisha shukrani kwa wateja wa bia ya Serengeti Premium Lager mara baada ya bia hiyo kushinda kinyang’anyiro cha bia ya kimataifa yenye viwango bora katika tuzo za “monde selection” za mwaka huu.