Mkazi
wa Tegeta Kibaoni aliyetambulika kwa jina la Libelius Ochungo
(Katikati) akipokea zawadi ya mfuko na fulana toka kwa balozi wa bia ya
Tusker Veronica Mbilinyi (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ambayo
ilifanyika katika baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam.
Baa hiyo ilitangazwa kama mshindi wa wiki wa promosheni hiyo
inayoendeshwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti.
Promosheni hii inaendelea pia katika mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza,
Moshi na Morogoro. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa Promosheni hiyo Gadner Habash.
Mkazi
wa Tegeta Kibaoni na mpenzi wa bia ya Tusker Bi. Leonarda Shayo
akiifurahia zawadi yake ya mfuko na fulana aliyokabidhiwa pale
promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilipofunga kambi ndani ya baa
ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki
wa promosheni hiyo ambayo inadhaminiwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya
bia ya Serengeti. Akikabidhi zawadi hiyo (Kulia) ni Balozi wa bia ya
Tusker Veronica Mbilinyi na (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni
hiyo Gadner Habash.
Mfanyabiashara na Mkazi wa Tegeta, Bw. Tungalaza Andrew akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombella wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani wikiendi ya Ijumaa iliyofanyika katika baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka baa ya wiki kwenye promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti.
Mkazi wa Tegeta, Uwanja wa Upanga ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Max Richard akijiandaa kupokea zawadi ya fulana toka kwa Meneja Masoko wa bia ya Tusker Bi. Nandi Mwiyombella (Kulia) wakati
wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika kiwanja cha baa ya
Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka baa ya
wiki kwenye promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker yenye lengo
la kuzihamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli
kwenye utoaji huduma kwa wateja. Promosheni hiyo ya nchi nzima
inaendelea pia katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Moshi, Morogoro na Mbeya.
Mkazi
wa Mtaa wa Yombo-Temeke, Bi. Asha Bakari akipokea zawadi yake ya fulana
toka kwa Afisa Masoko anayejifunza kwa vitendo toka Kampuni ya bia ya
Serengeti Bw. Josephat Shelukindo katika hafla ya kuipongeza baa ya
Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa
wiki kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Kiwanjani
inayodhaminiwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti.
Promosheni hii ya Tusker imejikita katika kuziunga mkono baa mbalimbali
za mitaa inayotuzunguka ili kuhakikisha kuwa zinatambulika kwa wateja wa
eneo husika na kufanya kweli kwenye utaoji wa huduma.