BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???

 
Mmoja wa wakurugenzi wa LG toka Korea, Bw. Billy Kim (Kulia) akizindua rasmi friji mpya ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish” katika banda la LG ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama “Sabasaba” anayeshuhudia (Kushoto) ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji Jaffer.

Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG Tanzania, Bi. Elizabeth Morris (kushoto) akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari hawapo pichani aina mpya ya friji ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish” wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya, katika viwanja vya maonyesho ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”. Kulia ni Mkurugenzi wa LG Mohan Kumar na mmoja wa wakurugenzi wakuu wa LG toka Korea Bw. Billy kim.

Meneja wa LG tawi la Nkurumah, Bw. Yasin Lodhi akiwaonyesha waandishi wa habari hawapo pichani ubora wa aina mpya ya friji ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish” iliyozinduliwa rasmi katika banda la LG kwenye maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es salaam.

Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari hawapo pichani aina mpya ya friji ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish”, wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya katika viwanja vya maonyesho vya sabsaba.

Mkufunzi mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) bidhaa nyingine za LG ambazo zipo kwenye ofa ya punguzo la bei ya asilimia 15 katika msimu huu wa sabasaba na ramadhani.


June 30, 2015 Dar es salaam: Katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani na maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es salaam maarufu kwa jina la Sabasaba, LG Tanzania imetangaza ofa kabambe ya punguzo la bei za bidhaa zake itakayodumu katika kipindi chote cha ramadhani na Sabasaba.
Wateja watakaonunua bidhaa za LG katika kipindi hiki cha ramadhani na Sabasaba watafurahia punguzo la bei la hadi asilimia 15 pamoja na ofa nyingine za kuvutia zikiwemo zawadi za bure, alisema Meneja mwandamizi wa LG, Mr. Kim Taehoon.
Mr. Kim pia alitumia fursa hiyo pia kuitambulisha friji mpya ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish” kwa mara ya kwanza kabisa katika soko la Tanzania na kuthibitisha kuwa kampuni ya Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) kuwa msambazaji rasmi wa bidhaa hiyo nchini.
Alisema friji hiyo ina nafasi kubwa na nyingi za kuhifadhia vyakula, uwezo wa kuzuia bakteria na hivyo kutunza vyakula katika hali ya usalama na wa kiafya, friji ina makabati yaliyojengewa kwa ndani katika milango yake, aina hii ya milango huja pamoja na kioo imara. Friji hii inatumia teknolojia mpya ya LG “Smart Inverter Compressor” ambayo ina uwezo wa kupunguza matumizi ya umeme hadi asilimia 36.
Aliongeza kuwa katika kipindi hiki cha maonyesho ya biashara ya Sabasaba, wateja wa LG watajipatia ofa kabambe pale watakapotembelea banda la LG kiwanjani hapo ambapo pia wataweza kupata bidhaa nyingine mbalimbali za LG ikiwemo friji jipya la milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish”
Bw. Kim amewashauri watanzania kuchangamkia fursa ya bidhaa hiyo mpya iliyoingia sokoni na kuwahakikishia kuwa watastaajabishwa na ubora na uwezo wa friji hilo huku akiongeza kuwa Friji hilo pia litapatikana katika maduka mengine yote yanayouza vifaa vya kielektroniki jijini Dar.
“Katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa ramadhani, watu wengi hutunza vyakula vyao kwenye mafriji na ni hulka ya wengi kuamka usiku kwa ajili ya kupata Daku, hivyo bidhaa hii itakuwa na manufaa sana kwao kwani ina uwezo wakulinda dhidi ya unyevunyevu na pia kutunza chakula katika hali ya usalama” alisema Kim.
Ofa hizi zitadumu kipindi chote za mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na Sabasaba, hii ni katika kuwapa wateja wa LG muda wa kutosha kujipatia bidhaa za LG zenye punguzo la bei
“LG Electronics daima inaendelea kuboresha mfumo wa teknolojia ili kuleta bidhaa zenye ubora na muonekana yakinifu ili kufikia viwango vya matumizi ya kimataifa na toka kuanzishwa kwake mwaka 1958, LG inaendelea kuzalisha bidhaa zinazoendana na mahitaji ya wateja wake na uingizwaji wa bidhaa hii mpya sokoni ni muendelezo wa matoleo yetu ya teknolojia ambayo yanatengenezwa na kuboreshwa kulingana na matakwa na mahitaji ya wateja wetu” alisema Mr. kim Taehoon