Kampeni maarufu ya Tusker Fanyakweli
Kiwanjani inatarajia kutimua vumbi wiki hii kwa wakazi wa jiji la Dar huku
ikitanua wigo wake mikoani baada ya kufanya vizuri kwenye kipindi chake cha
kwanza.
Kampeni hii inayoletwa kwenu na Kampuni ya
bia ya Serengeti imejipanga kusaidia baa mbalimbali za mitaa tunayoishi na kuzipigia
promo ya huduma zake kwa wapenzi mbalimbali wa kinywaji cha Tusker.
Akizungumza kuhusiana na mchakato mzima
wa Kampeni hiyo Meneja chapa bia ya
Tusker Bi. Sialouise Shayo alisema SBL kupitia chapa yake ya Tusker imejipanga
kutembelea baa zaidi ya 1000 kwenye miji yote mikuu nchini ikiwemo Dar es
salaam, Arusha, Morogoro, Moshi, Mbeya na Mwanza.
“Uamuzi wa kuongeza muda wa promosheni
hii ya Fanyakweli Kiwanjani ni kutokana na maombi mbalimbali hasa toka baa za
mikoani kufanyiwa promo/shindano kama hili kwenye baa zao”…alisema Sialouise.
Akifafanua zaidi kuhusu ratiba ya promosheni
hiyo kwa wakazi wa Dar na mikoani, Sialouise alisema taarifa rasmi ya
maandalizi ya promosheni hii itatangazwa kwenye vyombo vya habari vya mikoa
husika ili kuwajulisha wapenzi wote wa kinywaji cha Tusker kuhusiana na nini
kinaendelea.