Tarehe 06 Juni 2015 Dar es Salaam,
Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani, imechukua sura nyingine wiki hii
baada ya kumpata mshindi wa nne wa promosheni hiyo ambayo imebakisha muda wa
wiki moja tu kufikia kikomo.
Sura hiyo imejidhihirisha siku ya jumamosi baada ya “Kilwa road pub” ya
Kurasini kuibuka mshindi wa wiki wa shindano la Fanya kweli Kiwanjani
linaloendeshwa na bia ya Tusker kutoka SBL.
Utaratibu wa utoaji zawadi kwa baa zilizoshinda umekua ni kuwafanyia
promo za nguvu ambazo zinaambatana na zawadi za aina mbalilimbali kama vile;-bia
za bure, fulana za bure na bangili za mkono kwa wateja
Hadi mishale ya saa moja jioni Kiwanja hicho kilikua kimechangamka
vilivyo ambapo wapenzi mbalimbali wa kinywaji cha Tusker walifika kiwanjani
hapo kufurahia burudani ya mziki uliokua ukipigwa na kusikika moja kwa moja
toka redio E-fm.
Akiongea na waandishi wa habari waliofika kiwanjani hapo Meneja wa baa
hiyo Bw. Napoleon Mwanjelwa alisema “Nimefurahi sana kwa kuwa ushindi huu
umetuletea neema siku ya leo”. Akifananua zaidi Bw. Mwanjelwa aliongeza kuwa baa
hiyo haijajahi kuuza bia kupita kiasi kama siku hiyo na kuwashukuru mameneja wa
Tusker kuanzisha shindano lenye tija kwa baa za mitaa tunayoishi.
Akikabidhi zawadi ya fedha taslim kiasi cha Tsh 100,000/= kwa wahudumu wa
baa hiyo baada ya kufanya kweli kwenye upande wa huduma kwa siku hiyo, Afisa mauzo wa SBL eneo la Kurasini Bi.
Rahma Mjata alisema “Tunaipongeza
Kilwa road Pub kwa kuibuka mshindi wetu wa wiki na zaidi niwashurkuru mashabiki
walijitoa kuipigia kura baa hii”. Bi Mjata aliongeza kuwa baa hiyo imeshinda
baada ya mashabiki zaidi ya 50 kuipigia kura kupitia njia mbalimbali za mitandao
na pia kupitia kipindi cha Ubaoni kinachorushwa na redio E-fm.
“Hadi kufikia sasa baa zaidi ya 40 za hapa jijini zimeshindanishwa na
kuibua washindi 4 ambao ni; Toroka Uje bar ya Kimara, Yenu Bar ya Ubungo, New
Jambo Bar ya Mabibo na leo hii Kilwa road pub-Kurasini” alimalizia Bi. Mjata.