BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???

 
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa rasmi na wateja wa benki hiyo hivi karibuni. (Anayeangalia kulia) ni Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Prof. Joseph Semboja. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania, 16 June 2015National Microfinance Bank (NMB), Benki inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi nchini, imezindua rasmi familia ya kadi za benki “MasterCard Debit”, zikiwemo Tanzanite, Titanium  kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Kadi ya “First world Rewards”.  
Familia hii ya kadi hizi za benki zitahudumia wateja aina mbalimbali, ikiwemo asilimia kubwa ya wateja (Tanzanite), wateja wa kipato cha kati (Titanium) na wale wateja wa kipato cha juu (World Rewards) ikitoa huduma na faida mbalimbali mahususi kwa walengwa.
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa (katikati) pamoja wakurugenzi wa Benki ya NMB wakikishangilia kikundi cha sanaa kilichotumbuiza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumika kwa mara ya kwanza kwa wateja wake. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

“Pamoja na ukuaji wa kasi katika sekta ya malipo kwa njia ya elektroniki, wateja wetu wanazaidi kutafuta njia za haraka, salama na zenye unafuu kutumia katika malipo. Kukabiliana na wimbi hili, tumezindua familia hii ya kadi zinazokubalika kimataifa, na hivyo kurahisisha upatikanaji wa pesa zao kwa usalama popote walipo, Tanzania au nje ya nchi” alisema Ineke Bussemaker, Mkurugenzi mtendaji wa NMB.
Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam . 

Wamiliki wa kadi hizi za ‘MasterCard’ wataweza kutoa Fedha kutoka mashine za Miamala ya fedha duniani kote zenye alama ya “MasterCard Acceptance” ya fedha. Pia wataweza kulipia bili, kulipia umeme na Salio za simu, pamoja na kununua bidhaa mtandaoni kutoka maduka mbalimbali makubwa ndani na je ya nchi. 
Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumika hivi karibuni kwa wateja wake. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam. 

“Kadi za “MasterCard debit” zinakubalika na mamilioni ya wafanya biashara kutoka nchi Zaidi ya 210, ikiwa na maana kuwa wanaosafiri kwa ajili ya mapumziko au biashara wataweza kupata pesa zao popote pale, kwa urahisi kama wakiwa nyumbani” alisema Michael Miebach, Raisi, Mashariki ya kati na Africa, MasterCard. “muhimu Zaidi, kila muamala wa kitaifa na kimataifa unalindwa na usalama wa “masterCard SecureCode pamoja na EMV chip na Teknolojia ya PIN” ambazo hutoa usalama wa ziadakila mara mteja anatumia kadi yake mtandaoni au katika duka la kawaidia.”
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa akihutubia wadau wa benki ya NMB kabla ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Mastercard ya benki ya NMB ambayo itatumika rasmi kwa wateja wake hivi karibuni. Hafla iliyofanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro Hotel.

NMB pia inakuwa Benki ya kwanza Tanzania kuzindua kadi ya “MasterCard World Rewards”. Kadi hii inawapa fursa wamiliki kupata huduma za kipekee za kiamisha kama vilie ofa za ndege, malazi, kukodisha gari, vyakula, manunuzi, michezo na burudani kupitia “Mastercard priceless Cities and Priceless Africa Programmes”.
Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara tu baada Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin W. Mkapa kuzindua rasmi huduma mpya ya NMB Mastercard. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency, jijini Dar es Salaam.

“Hapa NMB tunaamini ni muhimu kufahamu mahitaji na matakwa ya wateja wetu, na kuwazawadia kutokana uaminifu wao. Tunayofuraha kuwa benki ya kwanza Tanzania kutambulisha mpango huu wakimapinduzi unaotoa zawadi kwa wateja wetu wa kipato cha juu huduma mbalimbali za kipekee za kimaisha, kupitia matawi yetu yaliyopo tayari na tawi letu jipya kabisa la “Private banking” litakalo hudumia wateja wetu wa kipato cha juu” alisema Bussemaker.
Wadau wa benki ya NMB pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumiwa rasmi na benki hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

Wamiliki wa kadi za “Worlds Rewards” wataweza kujipatia poinyti za uaminifu kila mara wanapotumia kadi zao. Pointi hizi za uaminifu zinaweza kukombolewa kwenye mashirika ya ndege zaidi ya 800 dunia nzima, kampuni za kukodisha magari an hoteli maarufu Zaidi ya 160,000 duniani.  
Wamiliki wa kadi zilizo kwenye familia hii, wataenedlea kufurahia huduma nyinginezo za NMB zikiwemo “NMB App, NMB Internet Banking, NMB E-Statement na NMB Mobile”.
-MWISHO-
Kuhusu NMB
National Microfinance Bank (NMB) ndio benki ya biashara  inayoongoza kwa huduma zote kamilifu hapa Tanzania ikitoa huduma mbalimbali za kibenki kwa kundi la wateja linalowakilisha vyema Tanzania nzima. Benki hii hutoa huduma kama za akiba, mialama pamoja na huduma za ufadili kwa watu binafsi, kuanzi kampuni ndogo hadi za kati, serikali, kilimo biashara pamoja na makampuni makubwa na taasisi. NMB pia ina jukumu muhimu katika sekta ya kilimo pamoja na maghala hapa nchini kupitia SACCOS na Amcos.

Katiaka Ubinafsishaji mwaka 2005, benki ilikuwa na wateja takribani 600,000, idadi hiyo ikiongezeka na kufikia millioni 1.8. Benki haikuwa na Mashine ya muamala (ATM) hata moja miaka mitano iliyopita, leo hii inamiamala Zaidi ya 600, ambayo ni asilimia 40 ya mashine zote Tanzania kwa ujumla. Benki inamatawi zaidi ya 170 na inapatikana katika asilimia 95 ya wilaya zote za kiserikali Tanzania. Nia ya benki hii ni kufikia asilimia 100 ya wilaya zote Tanzania

Fuatilia ukurasa wetu Twitter @NMBTanzania na upande wa Facebook NMB Tanzania