Ni Siku moja tu imepita toka msanii wa filamu nchini Kajala Masanja kufunguka ya moyoni juu ya Wema Sepetu na Petit Man na kueleza kuwa kamwe katika maisha yake ya hapa Duniani hawezi kusahau fadhila na moyo wa upendo ambao ulioneshwa na watu wao kipindi ambacho alikuwa na matatizo na jinsi walivyoweza kujitolea mpaka kufikia hatua ya kuweza kumsaidia katika matatizo ambayo alikuwa anakabiliana nayo kwa kipindi kile.
Kajala alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instgram na ndipo hapo alipoamsha hisia za mashabiki ambao wameanza kumuomba Wema Sepetu kumsamehe Kajala ili waweze kumaliza tofauti zao ambazo wanazo sasa.
"Binadamu tuliumbwa kuishi katika misingi ya ubinadamu na sio unyama kama waishivyo wanyama wa porini leo naomba kusema kutoka moyoni mwangu.. najua kabisa nina wazazi wangu ndugu zangu na zaidi sana mungu wangu ila kuna watu mpaka nakufa kamwe sintowasahau katika kuta za moyo wangu katika kipindi changu kigumu nilichopitia mlikuwa nembo na mboni kubwa katika kuokoa maisha yangu..
"Napenda kusema kuwa hata kwa haya yote tunayopitia bado ni madogo sana kuficha thamani yenu mliyoijenga juu yangu..nakumbuka sana mlipojitoa kwa ajili yangu mlipojinyima kwa ajili yangu mlipopigana kwa ajili yangu, mlivyofedheheka kwa ajili yangu yote hayo nayakumbuka na namshukuruu mungu kwani naona kabisa mliletwa duniani kwa sababu nyingi na moja ya sababu ilikuwa kuniokoa katika kipindi kigumu katika maisha yangu.
"Leo hii tarehe 25.5.2015 napenda kusema kwa Umma na zaidi kwa mungu wangu kuwa nawathamini nawapenda na nashukuruuu sana kwa yote mliyofanya juu yangu.. nawaombea kwa mungu muendelee na moyo huo huo kwani naamini kuna wengi bado wanawategemea ili kukomboa maisha yao kwa wakati aliyopanga Mungu. hata kitabu cha dini kilisema kuwa "huwezi kumpenda mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona" najua siku moja tutaishi kama zamani.." Aliandika Kajala
Baadhi ya mashabiki wameonesha kupenda jambo ambalo limefanywa na Kajala na kuona kuwa amefanya jambo la kiungwana sana na anastahili pongezi au msamaha kama kweli kuna jambo alitenda ambalo ndilo limeleta utofauti wao ndiyo maana mashabiki hao wamemtaka Wema Sepetu na Martin Kadinda kuweza kumsamehe ili waweze kuishi kama ambavyo walikuwa wakiishi mwanzo.
"Mwantumum Kilindi: Good sana my Kajala nimeipenda Allah atawasaidia mtaishi kama zamani mwenyezi Mungu kasema mara saba sabini na inapendeza binadam kushirikiana si unafiki binadamu haipendezi kununiana maana kila binadamu ataoza leo hii usimchukie binadamu mwenzako kwa kosa gani haswa lisilo sameheka minatafurahi endapo mtapatana wote na Aunt Wema na wewe Kajala ila marafiki sikuzote si wakumueleza undani wako namkishakua marafiki wa tatu ni unafiki utaendelea nawapenda wote, sote tutafukiwa hujui nani atatangulia leo hata kesho allah atawaongoza."
"Irene.Kimenye: Binadamu wote ndugu mlisahau kabisa kwamba ninyi ni kioo cha jamii nakumbuka kwenye kipindi cha mkasi ulichohojiwa ulikiri Wema ndiye aliyekufundisha biashara na mambo ya mtandao. Urafiki wenu watu wengi nikiwemo mimi niliupenda lakini haukufika popote mlichogombana mnakijua ninyi.Kama umekaa na ukafikiria na ukaona haya uliyoyaandika hakika Mungu atawaongoza na mtarudi kama zamani ingawa sio kwa ukaribu ule.
"Emelinaswebe: Wema msamehe mwezio jamani,haya ni maisha tu yanapita, mnabidi mmalizane"
"Jasleeee_ safi sana Kajala Mungu ni mwema siku zote amini kila jambo linasababu kwa Mungu. amini utayaweza yote katika yeye akupae uzima. hivyo iko siku wema atakusamehe na mtaendelea kama zamani kwani hizo nitofauti tu za kawaida mpendwa."
"Ajumysalum: Jamani huu ndiyo ungwana Kajala hongera sanaa @wemasepetu @new_kajala samehaneni bhana asante @ my shoga @pendojerry for the tag imenifunza kitu hii