
Tusker Lager kupitia kampeni yake ya “Fanya
kweli” wiki hii inawaletea wateja wake shindano la wiki lilopewa jina la “Fanya
kweli Kiwanjani”. Shindano hilo litahusisha baa mbalimbali za mitaani tunapoishi ndani ya
jiji la Dar Es Salaam.
Kampeni hii ya
“Fanya Kweli” imekua na lengo la kuhamasisha
watanzania kujitengenezea maisha mazuri ya baadaye kupitia juhudi zao
binafsi pamoja na msaada wa wadau ambapo kwa kiasi kikubwa imefanikiwa
kuhamasisha na kubadilisha fikra za watanzania wengi kupitia
vipindi na matamasha yanayolenga kuthamini watanzania wenzetu
waliofanikiwa
katika maisha na hivyo kuwapa motisha watu wengine kufuata nyayo zao.
Shindano hili ambalo litadumu kwa
takriban muda wa wiki tano, linatazamia kutoa zawadi mbalimbali kwa wapenzi wa
bia ya Tusker na baa zao wanazozipenda ambapo zaidi ya baa 50 jijini Dar es
salaam zinatarajiwa kushiriki kikamilifu kwenye shindano hilo. Kati ya baa 50
zitagawanywa kwenye makundi ya baa 10 kwa wiki ambapo zitapewa promo nzito wiki
husika kupitia kituo cha redio cha E-fm kwenye kipindi cha
“Ubaoni” kinachorushwa kati ya saa tisa mchana mpaka saa moja usiku na
watangazaji wake mashuhuri, Gardner G. Habash na Seth wataipa promo kampeni hii
nzima pamoja na kuwakumbusha wapenzi wa baa zinazoshindana kushiriki kwenye
kampeni hii.
Watangazaji hawa pia watagawana
baa 5 kati ya 10 zitakazo shindanishwa, kisha kuwaomba wasikilizaji wao
kuchagua baa 1 bora na baa itakayoibuka mshindi kituo cha radio cha E-fm
kitafunga kambi ndani ya baa hiyo na kuwafanyia sherehe pamoja na kukabidhi
zawadi mbalimbali. Watangazaji hawa pia watatoa maelekezo ya jinsi gani
wasikilizaji watakavyoweza kuzipigia kura baa wazipendazo na pia jinsi ya
kushinda zawadi ndogo ndogo zitakazotolewa kwa wasikilizaji wa kipindi hicho
cha redio.
Kupitia shindano hili, Tusker imedhamiria kusaidia katika kuzitangaza
zaidi baa maarufu za mitaani tunapoishi sambamba na kuibua sifa za huduma nzuri
zitolewazo na baa hizo huku pia ikionekana kama njia ya kuwaongezea mauzo kwa
ujumla. Kuna njia mbalimbali ambazo mashabiki wa Fanya kweli kiwanjani wanaweza
kuzitumia katika kuzipigia kura baa wazipendazo ambapo anachotakiwa mtu kufanya
ni kutembelea baa ya mtaani kwake na kunywa bia ya Tusker, kupiga picha na
kisha kuweka picha hizo kwenye kurasa za jamii (Facebook na Twitter) za Tusker
au kusikiliza E-fm kwa maelekezo zaidi.