 |
Meneja Vipoozeo na mwonekano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Baraka Mandara (Kushoto) akikabidhi
zawadi ya Tisheti kwa Bw. Seth Noel(Katikati) kama sehemu ya kurudisha shukrani
kwa wapenzi wa bia ya Tusker waliojumuika pamoja kwenye sherehe ya kuipongeza
baa ya wiki iliyofahamika kwa jina la “Toroka uje”. Baa hiyo iliyopo
Kimara-Korogwe jijini Dar es salaam iliibuka mshindi wa kwanza kwenye promosheni
ya “Fanya Kweli Kiwanjani” inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti
kupitia bia yake chapa Tusker.(Kulia) ni Mtangazaji wa kipindi pendwa cha
Ubaoni kutoka redio E-fm Bw. Gadner G. Habbash. Kampeni hii inatazamiwa kudumu
kwa muda wa wiki tano huku baa zaidi ya 50 za jiji la Dar es salaam
zikishindanishwa
|
 |
Mtangazi wa kipindi
pendwa cha Ubaoni kinachorushwa na redio E-fm Bw. Gadner G. Habbash (Kulia) akikabidhi
zawadi ya Tisheti na bia kwa mpenzi wa kinywaji cha Tusker Bw. Adrian Sengebere(Katikati)
wakati wa kusherekea ushindi wa baa ya “Toroka uje” iliyopo Kimara-Korogwe mara
baada ya baa hiyo kuibuka kinara wa kwanza kwenye promosheni ya Fanyakweli
Kiwanjani ambapo kupitia ushindi wao walifanyiwa sherehe ya nguvu na kampuni ya
bia ya Serengeti kwa udhamini wa bia yake madhubuti ya Tusker iliyofunga kambi
kwenye baa hiyo siku ya jumamosi na kuporomosha burudani ya nguvu kwa wateja
wake huku lengo likiwa ni kukitangaza kiwanja hicho kama kiwanja bora zaidi kwa
upande huo wa Kimara na kwa kufanya hivyo kuiongezea baa hiyo mapato yake. (Kushoto)
ni mhudumu wa bia ya Tusker Bi. Anneth Kimaro. Kampeni hii inatazamiwa kudumu
kwa muda wa wiki tano huku baa zaidi ya 50 za jiji la Dar es salaam zikishindanishwa. |
 |
Bi. Veronica Mbilinyi
(Kushoto) mwakilishi kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti akikabidhi zawadi ya
Tisheti kwa Bw. Johnston Liwale kama shukrani kwa mpenzi huyo wa Kinywaji cha
Tusker ambaye alijumuika na wadau wengine kwenye sherehe ya kuipongeza baa ya
“Toroka uje” iliyopo Kimara-Korogwe ambapo baa hiyo iliibuka mshindi wa kwanza
kwenye promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya
Serengeti kwa udhanmini wa bia yake madhubuti chapa Tusker. Kampeni hiyo
inatazamiwa kudumu kwa muda wa wiki tano huku baa zaidi ya 50 za jiji la Dar es
salaam zikishindanishwa. |
 |
Bi. Anneth Kimaro (Katikati)
akionyesha zawadi ya Tisheti na bia aliyokabidhiwa na mwakilishi toka SBL Bi.
Veronica Mbilinyi (wa pili kulia) wakati wa sherehe ya kuipongeza baa ya wiki
iliyofahamika kwa jina la “Toroka uje”. Baa hiyo iliyopo Kimara-Korogwe jijini
Dar es Salaam iliibuka mshindi wa kwanza kwenye promosheni ya “Fanya Kweli
Kiwanjani” inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake chapa
Tusker. (Kushoto) ni mtangazaji kutoka redio E-fm Bw. Gadner G. Habbash ambaye
anahusika kuipatia promo kampeni hiyo kupitia kipindi chake pendwa cha Ubaoni
kinachoruka siku za juma kuanzia saa tisa mpaka saa moja usiku. Kampeni hii
inatazamiwa kudumu kwa muda wa wiki tano huku baa zaidi ya 50 za jiji la Dar es
salaam zikishindanishwa. |
Dar es salaam, 16 Mei 2015 Shindano la Fanya Kweli Kiwanjani limeanza kutimua vumbi
kwa kuzishindanisha baa mbalimbali za jiji la Dar es salaam kama ilivyokua
imetangazwa hapo awali.
Mapema
jioni ya jana, wadhamini wanaoendesha shindano hilo Kampuni ya Bia ya Serengeti
kupitia bia yake cha Tusker Lager wakishirikiana na kituo cha redio E-fm,
walifunga kambi katika baa hiyo iliyopo Kimara-Korogwe jijini Dar na
kuporomosha burudani ya nguvu huku wakitoa zawadi mbalimbali kwa wapenzi wa
kinywaji cha Tusker waliojumuika kwenye hafla hiyo.
Kikubwa
kilichowavutia zaidi wateja waliofika kwenye baa hiyo ni huduma nzuri ya
vinywaji, vyakula, fursa ya kutuma salamu moja kwa moja kupitia redio E-fm
sambamba na zawadi kutoka SBL kama Tisheti na bia za bure za Tusker
zilizotolewa kwa wateja hao na mtangazaji wa E-fm Bw. Gadner kwa staili mpya
iliyojulikana kama Mupe Mureke.
Mmoja
kati ya wateja wa baa hiyo aliyejishindia Tisheti na bia za bure katika hafla hiyo
kwa jina la Wema Usiri (30) akizungumzia baa hiyo alisema… “Nimefurahi sana
baada ya kusikia “Toroka uje” imekua baa ya kwanza kushinda promosheni hii ya
Fanyakweli Kiwanjani kiukweli inastahili”. Bi Usiri aliongeza kuwa sababu kubwa
inayoifanya baa hiyo kupendwa sana ni kutokana na huduma zao nzuri hasa upande
wa vyakula, vinywaji sambamba na burudani za kila aina kama muziki wa bendi
unaopigwa kila ijumaa na jumamosi mahali hapo. Wengine walioibuka na zawadi za
bia na Tisheti ni Bwana na Bi Lema, Romana Mwikombe na Anneth Kimaro.
Kwa
upande wake Meneja Vipoozeo na mwonekano wa Kampuni ya Bia ya
Serengeti Bw. Baraka
Mandara aliyemwakilisha Meneja Chapa wa Tusker alianza kwa kuwashukuru wananchi
wa Kimara-Korogwe na wapenzi wote wa Kinywaji cha Tusker waliofika kwenye hafla
hiyo ili kusherehekea kwa pamoja ushindi wa baa hiyo. “Lengo kuu la Kampeni hii
ni kuziwezesha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli kwa
kuzitambulisha kwa wananchi ambao tunaamini kutokana na sapoti yao baa hizi
zitaongeza vipato.”
Bw.
Mandara aliendelea kwa kusema kuwa “Toroka uje” ndio baa ya kwanza kufungua
promosheni hiyo na kuwasisitiza wapenzi wa Kinywaji cha Tusker kuendelea kupiga
kura kwa wingi ili kuziwezesha baa za mitaa yao kushinda.
Promosheni
hii ya “FanyaKweli Kiwanjani” ni muendelezo wa Kampeni ya Tusker
“FanyaKweli” ambapo itadumu kwa takriban muda wa wiki tano huku zaidi ya
baa 50 za jiji la Dar es salaam zikipewa fursa ya kushiriki kwenye shindano
hilo. Kila wiki kutakua na mshindi mmoja kati ya baa 10 zitazokuwa kwenye
kinyang’anyiro. Ili kuiwezesha baa ya mtaa unaoishi tembelea baa hiyo kisha
burudika na kinywaji cha Tusker na piga picha nyingi uwezavyo na uipendekeze
baa hiyo kwa kuweka picha hizo kwenye kurasa za jamii (Facebook na Twitter) za
Tusker au kusikiliza kipindi cha ubaoni kinachorushwa na redio E-fm kati ya saa
tisa hadi moja usiku ndani ya siku za juma kwa maelezo zaidi.