Staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michel ‘Lulu’amesema kuwa nyumba aliyomzawadia mama yake siyo ya kuhongwa bali amejenga mwenywe.
Lulu alieleza hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha televisheni cha The Sporah Show.
Je lulu aliwezaje kujenga nyumba hiyo ya kisasa? Kwa kipato gani hasa anachokipata? Maswali haya yalilipelekea baadhi ya watu kudah labda alihongwa.
Lulu amelifungukia swala hilo kama ifuatavyo;
“Kiukweli ile nyumba nimeanza kujenga nikiwa bado mdogo sana, ni nyumba ya chini ya kawaida lakini nilikuwa najenga kidogo kidogo, kwamba leo nikipata laki nampa mama leo kaongezee hiki…kwahiyo ni kwasababu mtu hajui atashangaa Lulu kapata wapi hela za vuuup, lakini ni kitu ambacho kimeenda kidogo kidogo imechukua hata miaka minne..kwahiyo mtu atashtuka kwasababu ameiskia leo sasa ndo hivyo mtu ataanza kusema kahongwa hajui background.” alisema Lulu.
Lulu alimzawadia mama yake nyumba mwaka jana kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama yake kutimiza miaka 45 ya kuzaliwa.