BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???


Imelda Mtema
Baada ya kula viapo vya kutozikana, wasanii wawili wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel Grayson wamejikuta wakiangua vilio wakati wakipatanishwa na rafiki yao mkubwa ambaye ni pedeshee anayejulikana kwa jina la Daudi Mambya.

Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Daudi aliwaita kwa mwaliko wa mishikaki bila wenyewe kujua kinachoendelea.

Habari zilieleza kuwa, Daudi ambaye kwake huwa hawafurukuti, amekuwa akiumizwa mno na tofauti ya wasanii hao kwa sababu ni watu walikuwa wakipendana hivyo kugombana kwao kulikuwa kunaleta shida kwa marafiki zao wengine.
Imefahamika kwamba, Daudi alitumia ujanja wa kuzungumza na kila mmoja kwa wakati wake ambapo alibaini kuwa hakuna aliyekuwa tayari kupatana na mwenzake.

Ilisemekana kuwa, Daudi alitumia ujanja wa kitaalamu ili kila mmoja kumuweka sawa bila kujijua.
Unajua Daudi ni rafiki yao sana, sasa hakuwa anapendezwa na tatizo ambalo limejitokeza hivyo alitumia njia tofauti ili kuweza kuwakutanisha pamoja tena waweze kupatana,” alieleza mtoa habari huyo.

Ilielezwa kwamba Daudi alianza kwa kumtafuta Wema na kumpeleka Coco Beach akimuambia kuwa anataka akamnunulie mishikaki huku wakati huohuo akimwambia Aunt naye wakutane ufukweni hapo.Shushushu wetu alizidi kufunguka kuwa Daudi alitangulia Coco na Wema, huku akifanya mawasiliano na Aunt na baada ya muda, Aunt naye aliwasili huku kila mmoja akibaki katika mshangao usioelezeka baada ya kukutana uso kwa uso.

Sosi huyo alisema kuwa Wema na Aunt walipoonana kila mmoja alikuwa kimya lakini Daudi aliamua kuwasomea risala ndefu iliyomwingia kila mmoja.Mambo yakipokaa vizuri, wawili hao walishuhudiwa wakiwa wamekumbatiana huku kila mmoja akiangua kilio kilichochukua takribani nusu saa hivyo kufanya eneo hilo kuwa kama kuna msiba.

“Yaani mpaka Daudi mwenyewe alidondosha machozi baada ya Wema na Aunt kukumbatiana na kuanza kulia.
Yaani ilikuwa simanzi kubwa sana,” alimalizia shuhuda huyo.Akizungumza na gazeti hili, Daudi alisema kuwa aliamua kuwapatanisha wawili hao kwa kuwa alikuwa hapendezwi na tatizo hilo na kwamba wote ni rafiki zake.
Kwa upande wake, Aunt alifunguka ya moyoni:
Tulipokutana kila mtu alijua tatizo lake na tukaona ni mambo ya kijinga, ikabidi tuweke tofauti pembeni maisha yaendelee.”

Wema alisema: “Mambo ya kugombanagombana hayana msingi na kwa vile ni mtu mzima (Daudi) aliwakutanisha, nikaona yaishe.”Wema na Aunt ambao walikuwa marafiki wakubwa waliingia kwenye mgogoro hivi karibuni baada ya Wema kumtuhumu Aunt kuunga mkono shoo ya Zari All White Party ya mwanadada Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mpenzi wa aliyekuwa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

GPL