BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameeleza kushangazwa na hatua ya Serikali kuwapatia kazi ya ujenzi wa Bandari ya Mwambani mkoani Tanga watuhumiwa wa sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/07/Zitto-Kabwe.jpg
Amesema watuhumiwa hao wamepewa kazi hiyo kupitia Mradi wa Mwambani Economic Corridor (MWAPORC), ambao utagharimu Sh trilioni 54, huku kukiwa hakuna taratibu za utangazaji wa zabuni zilizofuatwa na Serikali.
Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara iliyofanyika katika miji ya Mafinga na Iringa mkoani hapa ambapo alisema Serikali imeipa kazi ya ujenzi Kampuni ya VIP Engineering and Management inayomilikiwa na James Rugemalira ambaye anahusika katika sakata la Escrow.
Zitto alisema ACT-Wazalendo wanamtaka Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta afanye uchunguzi kuhusu mradi huo wa Mwambani na achukue hatua kwa kile alichodai kuwa utapeli wa watu wa Escrow.
“Mwambani Economic Corridor Project hapakuwa na zabuni yoyote iliyotangazwa, na huu mradi umekuwa ukiandaliwa na Serikali. Sheria ya Private Public Partnership (PPP) imeweka utaratibu wa zabuni kwa miradi ya ubia na Serikali.
“Taratibu hazijafuatwa, hakuna zabuni iliyotangazwa kuhusu Bandari ya Mwambani, miradi mikubwa kama hii Serikali hutakiwa kutoa ‘guarantee’ kwa mikopo ambayo inachukuliwa.
“Hivyo kuhusika kwa Rugemalira wa Escrow na mwanasheria Cathbert Tenga wa Richmond kwenye mradi huu ni mwendelezo wa miradi ya kitapeli,” alisema Zitto.
Zitto ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema uzito wa mradi huo wa bandari unakwenda sambamba na reli ambayo itafika hadi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
Alimtaka Waziri Sitta kutoa taarifa kwa umma kwa kuwa taifa limechoshwa na miradi ya kitapeli.
MWANASHERIA ATOA UTETEZI
Akitoa taarifa kuhusu mradi huo hivi karibuni, msimamizi wa mradi huo ambaye pia ni Mwanasheria mashuhuri nchini, Cathbert Tenga, alisema utamilikiwa na Watanzania wenyewe na si watu kutoka nje ya nchi kama ilivyo katika miradi mingine.
“Sisi hivi sasa tunahangaika kuhakikisha nchi hii inasonga mbele kwani mradi huu hivi sasa upo katika hatua za awali za upembuzi yakinifu kwa kuwa na timu ya wataalamu, na ili jambo hili liweze kusonga mbele ni lazima siasa ziepukwe,” alisema Wakili Tenga.
Alisema kutokana na juhudi wanazoendelea nazo hadi sasa wamefanikiwa kupata benki ya Afrika Kusini, DBSA, ambayo itafanya kazi katika mradi huo mkubwa nchini.
Tenga alisema mradi huo wa MWAPORC utakuwa ni moja ya nguzo kwa uchumi wa taifa ikiwa Serikali itaamua ufanyike kwa kuwaunga mkono Watanzania wazalendo badala ya kujali wageni pekee.
MWIGAMBA NA UMASKINI
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba, alisema hali ya umaskini nchini imezidi kuongezeka huku viongozi wakiendelea kuponda maisha.
“Wakati Rais Jakaya Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 hali ilikuwa mbaya, lakini bado watu walikuwa na matumaini ya kurekebishiwa hali zao, leo anakaribia kumaliza kipindi chake cha uongozi, uchumi bado unamilikiwa na watu wachache.
“Tanzania ni nchi pekee inayochimba madini ya tanzanite, mazao yao Mirerani ni madini, lakini bado Serikali ilichukua ule mgodi na kuwapa makaburu kutoka Afrika Kusini huku Watanzania wakibaki watazamaji. Pia walikuwa wakichimba huku wakiweka maji yenye sumu huku Watanzania wakiendelea kufa kwa Ukimwi na njaa,” alisema
Mwigamba.
Alisema pamoja na tanzanite kuchimbwa nchini, lakini nchi ya Afrika Kusini imekuwa ya kwanza katika soko la dunia kwa kuuza madini hayo ikifuatiwa na Kenya huku Tanzania ikishika nafasi ya tisa.
Source:  Gazeti la Mtanzania