Samahani kwa haya kama yatawauzi wengine hasa mashabiki wa Wema Sepetu .. Najaribu kufikiria kwa sauti tu kama Wema Sepetu kwa kutumia umaarufu wake na jina alilonalo angefanya biashara mbali mbali kama zifuatazo nadhani angekuwa ni mmoja wa wanawake wenye pesa za kufa mtu :
1.Spa and Beauty Parlour za kisasa-Duka la Urembo lenye jina lake ambapo wanawake wanaenda kutengeneza kucha (manicure and pedicure), nywele, massage, waxing, stem bath ama sauna na mengine mengi
2. Hotel ama Restaurant yenye jina lake ambapo siku moja moja yeye na marafiki zake wanakuwa wanahudumia na kutoa huduma special kwa wateja
3. Maduka ya nguo, viatu na handbags za kike ambapo kila mara anakwenda nje kuchukua vitu vipya na kuvitangaza kupitia page yake ya instagram yenye zaidi ya followers laki tano
Kwa ufupi ana potential kubwa kwa upande wa biashara kwa sasa as anapendwa na watu wengi ....
Thats it if only i was in her shoes...Nimemaliza.....
 
Top