Neno ‘Impersonator’ ni neno linalotosha kumtisha msanii yeyote.
Unaposikia kuwa kuna mtu anatumia jina lako kupata vya bure inaweza
ikawa ‘Police Case!’ Lakini, je unafahamu kuwa Diamond alishawahi
kujifanya Z-Anto akapendwa na mrembo fulani aliyedhani yeye ni Z-Anto?
Kabla Diamond hajakuwa Platnumz, kabla hajapata umaarufu alionao sasa, Z-Anto ndiye aliyekuwa akitikisa ‘airwaves’ na ngoma kama ‘Mpenzi Jini’ pamoja na hit iliyomvukisha mipaka, ‘Binti Kiziwi.’ Wakati huo wasanii wengi Afrika Mashariki walivuma sana kwenye Radio kabla hata kufikiria kutoa Video. Nyimbo za Z-Anto zilitamba lakini wachache sana walijua sura yake ikoje.
Hii ndiyo ilimpatia Diamond ‘opportunity’ ya kujifanya Z-Anto na kula vya bwerere kutoka kwa waliodhania yeye ni Z-Anto. Akiongea katika Heka Heka za kipindi cha ‘Leo Tena’ kwenye Clouds FM, Diamond alifichua kuwa, “Unajua mara ya kwanza niliogopa….lakini baada ya kuona kila mtu niliyekutana naye ananiamini halafu kulingana na nakula vitu kiubwete nikajifanya Z-Anto.”
Swali ni je, alikuja kugunduliwa na kuchukuliwa hatua yeyote? Au je, Z-Anto aliipata hii habari? Hauhitaji kujiuliza ilikuaje, ingia kwenye channel yetu ya Mseto East Africa hapa upate uhondo kamili utakaokuchekesha na kukushangaza sana ;