Kwa mtu ambaye ametokea kwenye maisha ya kawaida kama Aggy, bila shaka
nafasi hiyo adimu aliyoipata angeitendea haki, either kwa kujiendeleza
kielimu au kibiashara. Ni mda mrefu umepita toka binti huyo mrembo apate
shavu la kuishi kwenye ardhi ya Madiba yenye kila aina ya starehe bila
kufanya kitu chochote cha maendeleo.
Ki ukweli Dada yetu huyu kajibweteka mno, hata kama umepata mwanaume
mwenye Pesa kama Bakhresa, kujituma muhimu. Umebahatika kupata Uraia uko
na watu ambao wanakusaidia kusogeza maisha mbele lakini naona mwenzetu
umekazana kupost picha za makalio mpaka tunaona kizunguzungu huko Insta.
Kuna watu wanatamani hizo nafasi usiku na mchana ila hawazipati. Mbaya
zaidi ni lugha ambayo unatumia siku hizi huko Insta yani hadi aibu
kuongea, mtu unakaa nchi za watu kwa miaka zaidi ya mitatu unashindwa
kufanya juhudi za kujua lugha za wenzetu ambao wameendelea? Sio wote
wanaoenda nchi za watu wanafanikiwa kimaisha ila pia kuna vitu
tunajifunza tunapotembelea nchi za watu either viwe vizur au vibaya.
Kuna watanzania wengi tu ambao wamefanya mabadiliko kwa kuzitumia fursa
za kutembelea nchi za watu na kuleta mabadiliko kwenye maisha yao na
jamii kwa ujumla, mfano halisi Sporah Njau na Watanzania wengine ambao
hawajulikani.
Tunajua wazi kuwa Elimu yako haitoshi na wala hauna kipato kikubwa cha
kuweza kusababisha uishi maisha bila kumtegemea mtu. Ila ni vizur
ukajikumbusha ulipotoka, umepata bahati jiongeze, maisha yanabadilika
ipo siku watu unaowategemea hawatakuwepo tena. Soma hata vi short course
vikusaidie kukabiliana na maisha au fungua hata biashara.
Bahati haiji Mara Mbili..
By Warumi