KABAANG! Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,
amedaiwa kumfumania ‘laivu’ mchumba wake Siwema akiwa kitandani na
‘serengeti boy’ wake ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja,
Ijumaa lina full stori.
NI MWANZA
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mwanzo mwisho, tukio hilo
lilichukua nafasi Machi 15, mwaka huu maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza
ambako mrembo huyo alikuwa akiishi, baada ya Nay kupenyezewa ‘ubuyu’
kuwa mrembo huyo usiku wa Machi 14 alionekana akiponda raha ndani ya
klabu moja iliyopo katika jengo la Hoteli ya Golden Crest.
“Wambeya walimpenyezea habari Nay, kesho yake asubuhi sana akatimba
Mwanza kwa ndenge na kumkuta laivu Siwema akiwa na seregeti boy wake
kitandani,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
AMPOKONYA SIMU, AWAPIGA PICHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, Nay baada ya kuwakuta wawili
hao wakiwa katika hali ya taharuki katika chumba cha nyumba hiyo ambayo
alimpangishia Siwema, alimpokonya simu mpenzi wake huyo na kuwapiga
picha za ushahidi wawili hao kisha akamchukua mwanaye kurudi Dar.
SIWEMA ATOKA NA KANGA MOJA
“Siwema baada ya kuona Nay amempokonya simu, alikurupuka akiwa na kanga
moja kisha kumfuata ili arejeshewe simu yake, Nay aligoma na kukwea
teksi akamuacha Siwema akilalama,” kilidai chanzo hicho.
NAY MSTARABU?
“Kiukweli Nay ni mstarabu sana maana hakuonyesha hasira za aina yoyote
pamoja na kwamba aliwafuma laivu, alitoka taratibu, hakufanya ugomvi
wowote kama watu wengine wanavyofanya pindi wanapofumania,” kilizidi
kudai chanzo chetu.
NAY AKWEA PIPA, ARUDI DAR
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Nay kufanikiwa kumuacha
Siwema na jamaa yake, alikwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupanda
ndege kurejea maskani kwake jijini Dar.
“Jamaa (Nay) hakutaka kuuweka usiku, alichokifanya ni kukwea pipa na
kichanga chake hadi jijini Dar na kwenda kumkabidhi mama yake,” kilisema
chanzo hicho.
Siwema.
NAY ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu baada ya kuzinyaka habari hizo, alimvutia ‘waya’ Nay
ambapo alipopatikana na kusomewa mashtaka ya kwenda kumfumania mchumba
wake, alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa undani lakini
akadai amemchukua mwanaye mikononi mwa Siwema kutokana na mchumba wake
huyo kuzidiwa na mambo yake.
“Sitaki kuzungumzia chochote kwa sababu sitaki kuonekana mbaya, ila
kiukweli nilienda Mwanza na kumchukua mwanangu na hapa ninapozungumza na
wewe, mwanangu yupo chini ya uangalizi wa mama yangu mzazi,” alisema
Nay.
SIWEMA KAFUATA SIMU YAKE
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, chanzo kilicho karibu na wawili
hao kilipenyeza ubuyu kuwa Siwema ameibuka jijini Dar kwa lengo la
kufuata simu yake ikidaiwa kwamba eti ina siri zake nyingi.
SIWEMA HAPATIKANI
Jitihada za kumpata Siwema kupitia simu yake ili aweze kufunguka kwa
upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa mikononi mwa Nay,
jitihada zinaendelea ili na yeye afunguke ukweli wa tukio hilo.
TUJIKUMBUSHE
Nay na Siwema wamedumu kwenye uhusiano kwa takriban miaka mitatu ambapo
wamefanikiwa kupata mtoto huyo mmoja. Awali, Nay aliwahi kuingia kwenye
mgogoro na kigogo mmoja ambaye alikuwa akimtaka mrembo huyo lakini
alifanikiwa kumuweka mikononi mwake kabla ya kumfumania na serengeti
boy.