Wakati hit single ya Diamond Platnumz, Ntampata Wapi inatoka mwaka jana, watu wengi waliamini kuwa wimbo huo amemwandikia ex wake, Wema Sepetu.
wpid-wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1.jpg
Tetesi hizo zilienea baada ya kubainika kuwa wawili hao wameachana tena. Hata hivyo Wema amedai kuwa si kweli.
“Leo nasema rasmi kuwa hii nyimbo hakuniandikia mimi,” Wema aliiambia Radio 5 ya jijini Arusha.
“Because nilikuwa naisikia hii nyimbo hata wakati tulipokuwa kwenye uhusiano amekuwa akiimba, akiindika kwahiyo ilikuwa tu ni moja ya nyimbo zake kama anavyoandika nyimbo zote lakini nadhani tu timing ya kutoka ndio kidogo imekuwa na utata because kaitoa timing ambayo watu wote wakadhani kamuimbia Wema but in real sense noo,” aliongeza Wema.
Msikilize zaidi hapo chini.Story imeandikwa na Bongo5
 
Top