Live! Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’, baada ya kukaa
muda mrefu akiwa ‘singo’ tangu aachane na staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, anadaiwa kupata mrithi wa msanii huyo
aliyetajwa kwa jina moja la Swedi.
Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina
kimedai kuwa, Penny na Swedi wanaishi pamoja maeneo ya Mwananyamala
jijini Dar na wamekuwa wakioneshana mahaba nilegeze hata mbele za watu
huku mara kadhaa wakitupia picha zao za pamoja kwenye mitandao ya
kijamii.
“Hivi ninyi mnajua kuwa Penny kapata mrithi wa Diamond? Kama hamjui basi hiyo ndiyo habari ya mjini.
“Kwa taarifa yenu wanapika na kupakua na hakuna asiyejua hilo, kama vipi fuatilieni mtapata ukweli,” alidai mtoa habari huyo.
Katika kujiridhisha, waandishi wetu walianza kufuatilia kwa kufika
kwenye nyumba anayoishi Penny na kukuta imefungwa ila baadhi ya majirani
walidai kuwa, wanajua uhusiano wa Penny na Swedi kwani wanawaona kila
siku wakiingia na kutoka.
Penny alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi ili afunguke juu ya
hilo, iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa sms hakujibu hadi
tunakwenda mtamboni hivyo jitihada za kumpata ili aweke mambo sawa
zinaendelea.