BONGOCLAN Tanzania

Website yetu ipo katikamatengenezo

Copyright © BongoClan Tanzania™ | Published By Gooyaabi Templates | Powered By Blogger
Design by WebSuccessAgency | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com

HABARI ZILIZOSOMWA SANA WIKI HII

Wema ni kweli anavuta Bangi???

Leo kuna mtu kaniambia msome Mange kaongea kitu kizuri sana, nikampuuza ila aliponipa brief ikabidi niingie kumsoma.. Kwa kweli huyu mama uwa simkubali mpaka nakufa ila kaongea kitu cha msingi nimeona nikilete hapa ili wasanii wanaochungulia hapa ila wanajifanyaga huko JF siingiagi siasa tupu kumbe wana hadi Senior ids nao wapate darasa kwetu sisi tulio kando ya mchezo.

http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2012/08/Kina-na-Diamond.jpg Mange kaongelea wasanii wa bongo fleva na kupwaya kwenye ubunifu, akimwongelea zaidi Ali Kiba na singo yake mpya...Ntakuwa namnukuu. Penye maandishi ya bluu ni yeye sio mimi


I like Ali Kiba’s music but I think he needs to grow kimuziki. Mie naona toka arudi kwenye gemu nyimbo zake zimeshuka kiwango sio nzuri kama za zamani… Au labda tuseme yani nyimbo zake zote ni vile vile yani hazina tofauti.Yani they sound identical.Anabadilisha vitu vidogo vidogo sana

Hili nakubaliana na wewe Mange, Kiba wa sasa uwezi kumfananisha na wa Nakshinakshi au Cinderella.. Sasa hivi beef ndio linambeba sio quality ya muziki wake, mfano hii singo kiukweli kwa mtu anaejua muziki mzuri ata ajifanye kusema ni ngoma kali moyoni ukweli anaujua. Haya mambo ya kubebwa na beef yana mwisho wake. Ilimtokea Juma Necha, alibebwa sana na beef yake na kina chege akabweteka akaanza kutoa nyimbo chini ya kiwango sijui ndege tunduni sijui vitu gani. Ishu ikaja beef ilipokufa ikambidi awashawishi mashabiki na talent yake ikawa ndio mwisho wa Necha rasmi, tunaomba Kiba asifike huko.

hata besti ake Diamond pia nyimbo zake zimeanza kushuka kiwango…. Mie naona tatizo lipo hapa

Na Diamond nae nyimbo yake ya mwisho nitampata wapi haikuwa na viwango vya Diamond tunaemjua wa Mawazo, Ukimwona, Kesho nk.. Nafikiri Diamond kilichomwangusha ni ubize wa ratiba yake, hivyo kutulia kufanya kitu kizuri inakuwa ngumu pia presha ya ugomvi. Ila bado anaweza kufanya maajabu.
Mie naona ndo kama hawa vijana, wameshaandika all the best stuff they have sasa material zimekwisha inabidi wafanye tu ili mradi watoe new single…. Yani kwa Ali Kiba kwa jinsi alivyo under pressure sababu ya hiyo ya likinganishwa na Diamond naona hii new single imemwangusha kabisa yani na sasa ni dhahiri kuwa yeye ni number 2.

Presha ya mashabiki ni mbaya sana, wao wanataka kitu cha kupata kusema na kinaweza kisiwe kizuri ila wakakishabikia tu. Laakini unaweza kuicontrol kama mjanja ...Pia msanii inabidi uwe na kauli na wewe tatizo Ali kapata management mpya ila imekaa kizungu sana, mswahili bwana mpeleke kiswahili tu mambo ya kushutia video uzunguni wakati kisa cha uswazi wabongo utawazingua tu...ni sawa na hii video ya huu wimbo akafanyie kwenye mabarafu mbele.

VANESSA MDEE na JUMA JUX wanaface the same problem. Yani Vanessa na Juma Jux wana swaga za hatariiiiiiiii, yani wamekaa kimamtoni ile mbayaa ila tatizo ni nyimboooooooo, nyimbo hazina viwango vileeeee

Tatizo la Jux sio nyimbo Jux hana talent ya kuwa mwanamuziki star bali ana mikogo mingi ndio inambeba, Vanessa tatizo lake ni kuyumba na kutojua anataka nini ndio maana anaacha RnB anaanza kuimba kama Linah, Mwasiti, Recho ambao kiukweli wamechosha kusikilizwa sababu wadada wa THT wote ni kama wanaimba kitu kimoja na sababu kubwa mtunzi wao ni mmoja ambae Vanessa ameanza kumtumia asipoangalia ataishia njiani.. Radha za THT zimetosha ndio maana hata Ruge anataka kuifunga, ni kama imestuck.

Well, kunapokuwa na tatizo lazma tutafute na suluhisho… Tumeshajua tatizo sasa hivi ni uandishi wa nyimbo sio kwamba hawajui kuimba kama zamani. Talent zao zipo pale pale au hata labda zimeongezeka kutokana na experience ila problem is hawana tena material ya kuandika nyimbo
Hapa ndio pagumu kwenye muziki wa bongo, msanii atakubali kila kitu lakini sio kuandikiwa yaani wanaona kuandikiwa nyimbo ni aibu kubwa sana matokeo yake wanashindwa...Ila kiukweli wasanii inabidi wabadilike waanze kuandikiwa nyimbo mtu anasound vile vile miaka na miaka msikilize AY, MwanaFA, Benpol, TundaMan, TID, Dully nk akitoa wimbo mpya ni kama umeshawai kuusikia sababu kicwa kimeshachoka hakina jipya japo uwezo bado wanao.

Kuna wasanii wameandikiwa nawafahamu wakaja kama wapya mfano Shaa, Feruzi na kibodaboda, Aslay, hawa wote wanaandikiwa na Fela..Mama Ntilie Rayc na wale wapemba aliandika Adam Juma, zipo nyingi.
wasanii wetu ambao wameshajenga majina yao wasikubali kushuka kwa kung’ang’ana kuandika nyimbo zao wenyewe. Waanze kutumia professional writters ili waendelee kubaki kwenye gemu

Wasanii kukweli wawe profesheno, na hata maprodyuza wao wawe maprofesheno kuna nyimbo zina makosa mengi ila zinatoka sababu prodyuza hajui muziki anachojua ni kupiga mdundo baas, na wasanii wanakimbilia kwa awa maprodyuza underground sababu wanawarekodia bure..

Unasikiliza nyimbo ina kelele ila inapigwa daily redioni, big up kwa majani asingekuwa anajali profeshen yake huu muziki ungekuwa nyuma sana studio yake aliita wataalam kina bizman, kina raja wamsaidie mambo ya kimuziki wasanii wasio na talent ila walitaka kulazimisha fani kibabe aliwachapa sana ikawa kupitishwa na majani ni kama umefuzu hii ilisaidia kama screening flan ila kiukweli tunaitaji usiriaz ukiangalia muzki ni kama umefika kileleni unaanza kushuka watu wanaanza kukimbilia video wawe kama fulani ila muziki mbovu kama kina Temba sijui ndio nini kile wameimba..

Watu kama kina tundaman au nahreal sio waimbaji kabisa ila wasanii wangeheshimu watunzi wale jamaa wamngekuwa kwenye mastudio wanaandika tu. Kuna watu wapo kitaa na mishe zao zingine ila wana talent hatari maofisini huko wangefanya hii kama part time kulikwa kuwa na watu wale wale hakuna ubunifu..


Nawashukuru kwa kusoma gazeti langu ila linawahusu zaidi wasanii kama unalakuongzea welucamu kama huna potea usilete ushabiki wa maandazi mie nimemwaga facts tu sio ushabiki na unawausu wasanii zaidi..


Imeandikwa na Matumbo kutoka Jamii Forums