Msanii anayefanya vizuri kunako bongo movie, Jacob Steven maarufu kama
JB, hivi karibuni amekwaa scandal mpya ambayo imemshushia HESHIMA kama
sio kumpunguzia credit ndani ya tasnia hiyo.
Msanii huyo maarufu amekumbwa na scandal hiyo baada ya muvi yake mpya kutoka inayofahamika kwa jina la MZEE WA SWAGA.
Muvi hiyo inayofanya vizuri sokoni inasadikiwa kukopiwa na ku paste kama
ilivyo na moja ya movie maarufu kutoka bollywood inayofahamika kwa jina
la "Ladies VS Ricky Bahl".
Akizungumza kupitia kipindi cha take one, Zamaradi Mketema amethibitisha
usanii huo uliofanyika na kampuni maarufu ya JERUSALEM inayomilikiwa na
JB, Kuwa karibia scene zote zilizochezwa na Filamu ya "mzee wa swaga"
imeiga kama ilivyo kuanzia story hadi idadi ya waigizaji wakuu kutoka
kwenye filamu hiyo ya kihindi iliyotoka mwaka 2011.
Mtangazaji huyo amelaani vikali utapeli huo uliofanyika na kampuni ya JB
huku akijifanya yeye ndiye mtunzi na mwandishi wa story hiyo wakati
ukweli anaujua mwenyewe.