
“WAKATI WA KUIBUKA NA USHINDI MNONO KAMPENI YA ‘TUTOKE NA SERENGETI’
NI HUU”….YASEMA SBL
Dar es Salaam,
Tanzania: 04th Februari, 2015. Kampuni ya pili kwa ukubwa katika
utengenezaji wa pombe hapa nchini imeeleza kwamba kampeni yake inayoendelea
ya “Tutoke na Serengeti” inaelekea ukingoni. Kwa kigezo hicho, kampuni
hiyo imejipanga kumaliza kampeni hiyo kwa kishindo na njia ya kipekee
kwa kuhakikisha kwamba washindi wengi zaidi wanapata nafasi ya kujishindia
zawadi mbalimbali ambazo ziliorodheshwa hapo mwanzo.
Akiongea na waandishi wa habari ndani ya makao makuu ya Kampuni hiyo
yaliyopo Chang’ombe-Dar es salaam, Meneja Chapa wa bia ya Serengeti
Premium Bw. Rugambo Rodney alizitaja baadhi ya zawadi ambazo zinasubiri
washindi wengi zaidi kuzinyakua kama;- Limo Bajaj, safari ya kutembelea
mbuga za wanyama ijulikanayo kama “Mtoko wa mbugani”, fedha za papo
kwa hapo, bia za bure ambazo zinapatikana katika maeneo yote ya mauzo
nchi nzima pamoja na bia za punguzo.
“Ninafurahi kuona kwamba promosheni hii imepeta mwitikio mzuri Tanzania
nzima na kama kampuni tunajivunia kwa kuweza kutoa zawadi mbalimbali
kwa wateja wetu kama shukrani kwa kuwa pamoja na sisi…. Ninachoshukuru
zaidi ni kwamba zawadi nyingi tulizotoa zimeweza kuongeza vipato kwenye
maisha ya washindi wetu... Bado naamini kuna watanzania wengi ambao
wanatamani kutembelea mbuga za wanyama, kumiliki Limo Bajaj au hata
kujishindia fedha taslimu.”
Rodney aliongeza kwamba muda bado bado upo na wakati ndio huu, ingawa
zimebaki wiki tatu tu kwa wateja kujikusanyia zawadi hizo.
Aliendelea kuwakumbusha wateja kwamba, kushinda zawadi hizi ni rahisi
sana. Unachotakiwa kufanya ni kununua kinywaji cha Serengeti Premium
Lager, ambacho ndio kinywaji rasmi kinachodhamini kampeni hiyo na mteja
aangalie chini ya kizibo ambako atakuta namba ambazo zinatakiwa kutumwa
kwa njia ya SMS katika namba 15317 na moja kwa moja atakuwa ameingizwa
katika droo na kuwa katika nafasi ya kujinyakulia zawadi hizo.
SBL pia ilithibitisha mbele ya waandishi wa habari kwamba tayari imeshakabidhi
Limo Bajaj tano kwa washindi mbalimbali, wawili kutika mkoa wa Kilimanjaro,
mmoja kutoka mkoa wa Morogoro na wawili wengine kutoka mkoa wa Dar es
Salaam. Pia wengi wakiwa wamejishindia safari za kutembelea mbuga ya
wanyama ya Serengeti kwa watu waili, Fedha taslimu Tshs. 100,000 zimeshatolewa
kwa washindi zaidi ya 15 kila wiki na bia za bure kwa washindi mbalimbali
katika kipindi chote hiki cha kampeni.
Takwimu pia zimeonyesha kwamba washindi wengi wa “Tutoke na Serengeti”
wametoka mikoani na ambayo ni dalili nzuri ya kuonyesha kuwa kampeni
imepata muitikio mzuri nchi nzima.
Kampeni hii ya nchi nzima ilizinduliwa
rasmi na SBL ikishirikiana na BPESA miezi mitatu iliyopita ikiwa na
lengo la kuwazawadia wateja kila wiki katika droo zilizokuwa zikifanywa
na SBL chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya bahati nasibu Tanzania.
Siri kubwa ya ushindi katika promosheni imekuwa ni kutuma namba maalum
zilizo chini ya kizibo kwenda katika namba 15317 mara nyingi iwezekanavyo ili kutengeneza nafasi ya kushinda
Limo Bajaj na zawadi nyingine nyingi. Hata hivyo mshiriki anatakiwa
awe na umri wa miaka 18+ na anunue bia ya Serengeti Premium Lager tu.
KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA:-
Kurasa za Serengeti premium Lager Face book/Twitter na YouTube kwa
video.
KUHUSU SERENGETI BREWERIES LIMITED
Serengeti Breweries Limited inajihusisha na utengenezaji, uandaaji,
uuzaji na usambazaji wa vinywaji vya kimea na shayiri na uwele hapa
Tanzania.
Ikiwa na makao makuu yake hapa Dar es Salaam, bidhaa za Serengeti
ni pamoja na:- Serengeti Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager,
Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The
Kick na Guinness®..