VANESSA MDEE AZIDI KUMCHANGANYA JUX, TAZAMA PICHA ZAO WAKILA BATA AFRIKA KUSINI
Vanessa Mdee na Jux wote wapo nchini Afrika Kusini walikoenda kufanya video ambayo hata hivyo hawajasema ni ya wimbo gani na kwa mujibu wa picha wanazopost kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wanapeana kampani ya nguvu.
Hawajawahi kukubali hadharani kuwa ni wapenzi lakini picha zinaonesha wazi kuwa mastaa hao wapo kwenye dimbwi zito la mapenzi.
Kupromote wimbo wake mpya ‘Nikuite Nani’, Jux amepost picha akiwa na hitmaker huyo wa ‘Hawajui’ anayeonekana ‘akimchumu’ kwenye paji la uso.
Kabla ya picha hiyo, Jux alipost nyingine kadhaa akiwa na mrembo huyo katika pozi ambalo huwezi kuuliza kama ni marafiki tu.!
Hivi karibuni Vanessa Mdee alifunguka kuhusu uhusiano wake na Jux na kusema: "I actually I like to keep my private life private. Nadhani kuna baadhi ya mambo ambayo hayahitaji majibu.”
Jux na Vanessa wameongozana na Weusi na Navy Kenzo kwenye safari hiyo ya South.