Safari ya Ommy Dimpoz kuelekea Vegas,Marekani kwa ajili ya kupiga show imeishia Airpoet ya Marekani,baada ya kuzuiwa kuingia Marekani na kurudishwa na ndege inayofata
Habari zilizotufikia ni kuwa Dimpoz amerudishwa na kukataliwa kuingia ndani ya Marekani kwa kushindwa masharti ya Visa,ambapo Visa ilikuwa sio Visa inayomruhusu kufanya Show na hivyo kumtilia shaka.

"Tangia tulivyoachana ile ijumaa nilivyompeleka Airport,hatujawasiliana mpaka leo asubuhi ndiyo amenitumia meseji kwa sababu mi mwenyewenilikuwa namtafuta simpati,kwa hiyo na mi mwenyewe nilikuwa na wasiwasi sababu sio kawaida yake,siku zote waga akisafiri anapofika tu lazima aniambie kwamba nimefika salama sasa safari hii nimeona kimya,Ila leo ahsubuhi kwenye majira ya saa tatu amenicheki kuwa yupo njiani anarudi,anaingianleo usiku kwa hiyo mpaka kesho mtakuwa na jibu,haja nieleza kwa nini,aaaaah mi nnachojua yeye anavisa ya marekani ya mwaka mmoja kufanya kazi"alisema Meneja wake Mubenga
 
Top